MBUNGE wa Korogwe vijijini Mh. Timotheo Mnzava amewataka wananchi wa jimboni kwake kuwa na uthubutu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuipa nguvu serikali ili wapate kipaumbele katika kukamilisha miradi yao. 

Ameyazungumza hayo akiwa katika ziara yake ya kata 29 ndani ya jimbo hilo ambapo ilianza tarehe 1 Disemba na kutarajiwa kumalizika tarehe 15 Disemba 2018. 
Aidha kufuatia kero na changamoto za jimbo hilo kuwa nyingi, Mnzava amewaomba wananchi kuainisha vipaumbele ili kurahisha utatuzi wa kero hizo kuwa katika mtiririko unaofaa na kuepusha kugusa kila kero na hatimae kushindwa kuzimaliza kwa wakati. 
Aidha katika kata nne za Kalalani,Mashewa,Kizara na Foroforo ambazo tayari amezipitia, Mnzava ameahidi jumla ya Mifuko ya Simenti 270, ambapo katika mifuko hiyo 250 itatumika katika sekta ya afya na mifuko 20 katika sekta ya elimu pamoja na nondo 45 zitakazotumika kwenye ujenzi wa zahanati katika kata ya Foroforo. 
Aidha Mnzava amewataka wananchi kuondoa ukanda na ukabira ambao unapelekea kukwamisha shughuli za maendeleo ya korogwe vijijini na kuwaasa waishi katika misingi aliyoiachia baba wa taifa Mwalimu Nyerere juu kutanguliza utanzania na kuachanana tabia ya kubaguana kwa makabira. 
Aidha kufuatia ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni, Mnzava amewataka wanachi kuunga juhudi za rais wa awamu ya tano dkt. John Magufuli anzozifanya katika kuboresha sekta ya afya, elimu pamoja na miundombinu akiwa na lengo thabiti la kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...