Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NCHINI Marekani, Mjini Phoenix katika kliniki ya shirika la afya la Hacienda mwanamke mmoja aliyekaa mahututi (Koma) kwa miaka 10 amejifungua mtoto wa kiume katika kliniki hiyo.

Shirika la utangazaji la CNN nchini humo limeripoti kuwa Disemba 29 mwanamke huyo ambaye hakujulikana kama mjamzito hadi alipoonesha dalili za kujifungua, alijifungua mtoto wa kiume na polisi wa wameanza uchunguzi kwa udharilishwaji huo wa kingono kwa kutaka vipimo kwa damu (DNA) kwa wanaume  wanaofanya kazi kituoni hapo na taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa na Sajent. Tommy Thomson ilisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa kuwa amedharilishwa kingono alikaa kituoni hapo kwa muda mrefu katika kituo hicho cha Hacienda akipatiwa matibabu baada ya kupata tatizo hilo miaka 14 iliyopita.

Aidha imeelezwa kuwa hali ya mtoto aliyezaliwa ni njema kabisa na ulinzi katika kituo hicho umeimarishwa hasa kwa wanaume ambapo hawaruhusiwi kuingia Hacienda bila kuambatana na wasaidizi wakike.

Kliniki hiyo imelaani vikali tukio hilo na tayari mkurugenzi mkuu Bill Timmons ameachia madaraka mapema Jumatatu.

Hacienda ni kliniki maarufu nchini Marekani kwa kuhudumia watu wenye magonjwa sugu, watoto wachanga na watu wenye ulemavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...