Na Ripota wetu, blogu ya Jamii 

Uongozi wa klabu ya Yanga umebainisha Kiungo Mohammed Issa 'Banka' aliyekuwa akikipiga kandanda Mtibwa Sugar amebakisha wiki tatu amalize adhabu yake ya miezi 14 aliyofungiwa na FIFA kutokana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu akiwa mchezoni. 

Banka aliyesajiriwa na Klabu ya Yanga msimu huu 2018 -19 ambaye pia hajaitumikia hata mara moja timu hiyo kutokana na sakata hilo, ataanza rasmi kuvaa uzi wa Yanga February 08 2019 adhabu yake itakapokuwa imemalizika.

Uongozi huo unasema kuwa Mchezaji banka tangu mwezi uliopita aliruhusiwa kujifua na kikosi cha Yanga kujiweka sawa kabla adhabu yake haijamalizika na kurejea dimbani.Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kuvutiwa na kiungo huyo akimsifu kuwa ni aina ya wachezaji anaopenda kufanya kazi nao.

Baada ya kocha huyo kufanya nae mazoezi kwa Muda mfupi amesema kuwa amebaini kiungo huyo atakuwa msaada mkubwa kwa kikosi cha Yanga ambacho sasa kimeweka dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

"Nimevutiwa sana na Banka ukimuona uwanjani mazoezini utagundua kwamba ni mchezaji ambaye licha ya kuwa nje kwa muda mrefu lakini alikuwa akizingatia nidhamu ya mwili, nilikuwa nahitaji sana mtu kama huyu katika timu yangu, " amesema Zahera

Vile vile kocha Zahera ameeleza kuwa katika mazoezi ya Yanga Banka ameonyesha uwezo mkubwa katika majukumu ya ukabaji, kuchezesha timu na hata kufunga vitu ambavyo vitaipa nguvu timu yake katika mzunguko wa pili.
Mchezaji Mohammed Issac Banka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...