Aeleza itafika kokote madini yanakochimbwa pasipo vibali halali

Na Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.

Biteko ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.

Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila na wajumbe aliambatana nao wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katikati ya hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu 
Pori kwa pori mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha, kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani 
Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani katika hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu. 
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Wizara ya Madini katika wilaya yake ya Meatu 
Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Fredy Mahobe akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya ujumbe kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Joseph Eliaza Chilongani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Meatu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...