Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetangaza kukamilisha mchakato wa ufumbuzi wa madeni ya iliyokuwa Benki M ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukwasi na hivyo kuihamishia katika Benki ya Azania Limited.

Akizungumza leo Januari 15,2019 jijini Dar e Salaam Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk.Bernard Kibesse amesema kuwa BoT kwa mujibu wa  mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 59(4)cha sheria ya mabenki na tasisi za fedha ya mwaka 2006 mchakato wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M umekamilika na madeni kwa madeni yake kuchukuliwa na benki 
nyingine kama njia ya ufumbuzi wa matatizo.

"Hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(20)(h) cha sheria ya Mabenki na Tasisi za fedha ya mwaka 2006 ,benki kuu imeamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria (aquisition by Operation of the law) mali na madeni yote ya bank M kwenda Azania Bank Limited,"amesema Dk.Kibesse.Ameongeza kuwa kwa sasa Benki kuu,Azania Bank Limited na wadau wengine wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Limited.

Pia wateja wenye Amana na wadai wengine wa Bank M watataarifiwa tarehe ya kuanza kupata huduma za kibenki kupitia Azania Bank Limited.Kwa wateja wenye mikopo amesema wanatakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao huku akisisitiza kuwa Benki Kuu inawaakikishia kuwa Azania Bank Limited itakuwa na Mtaji na Ukwasi wa kutosha katika kuwahudumia wateja wake na wateja wapya kutoka Bank M baada ya kuchukua mali na madeni ya benki hiyo, hivyo Azania Bank inatarajiwa kuwa na mtaji wa Sh.bilioni 164.

Alipoulizwa jitihada gani zimefanywa na Benki Kuu ili kuinusuru Benki M , Dk.Kibesse amesema kuna hatua mbalimbali ambazo zilifanyika ikiwa pamoja na kufanya vikao vya mara kwa mara kati yao na benki hiyo lakini kutokana na kutokuwa na mtaji wa fedha wameamua kuhamisha mali na 
madeni yake Benki ya AZania.

Hata hivyo amefafanua kuwa Benk M haikuwa imefikia pointi ya ukwasi huku akisisitiza kuwa kilichofanya Benki Kuu kuiweka Benk M chini ya usimamizi wake na kisha kuamua kuhamisha mali na madeni Benki ya Azania imetokana na tatizo kubwa la ukwasi.

Kuhusu deni lililokuwa Benki M, Dk.Kibesse amesema kulikuwa na deni ya Sh.bilioni 618 na kwa mazingira hayo ilikuwa vigumu kwa walioweka fedha kutaka kuchukua fedha na hivyo Benki Kuu moja ya jukumu lake ni kuhakikisha inaangalia hali hiyo kwa kuhakikisha wateja wanalindwa.

"Ndio maana tumesema Mkurugenzi Benki ya Azania atakapokuwa amekamilisha tararibu zote za kisheria, mteja ambaye alikuwa anataka huduma atakwenda na atahudumiwa na ile fedha ya ada ambayo mhusika alikuwa ameikosa ataipata,"amesema Dk.Kibesse  
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Dk .Bernard Kibesse akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuhamisha amana zote za Benki M na Madeni yake kwenda Benki ya Azania.
 Mkurugenzi wa Benki ya Azania Katikati Mwenye Tai Nyekundu akiwa na wadau wengine wa Masuala ya Kibenki waliohudhuria Mkutano wa BOT na Waandishi wa Habari
 Mwandishi wa Habari Kutoka Gazeti la Nipashe, Beatrice Moses akiuliza Swali kwa Gavana juu ya Mchakato wa kuhamishwa kwa benki hiyo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo ulikuwa ukitangaza maamuzi ya kuhamisha Benki Mkwenda Azania Bank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...