Na Ripota Wetu

INASIKITISHA ! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea tukio la kushambuliwa kwa Hoteli ya kifahari ya DusitD2 nchini Kenya.

Tukio la kushambuliwa kwa hoteli hiyo iliyopo eneo la 14 Riverside jijini  Nairobi nchini Kenya limetokea leo Januari 15,2019. Shambulio hilo limeibua hofu na taharuki kwa wananchi wengi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa wakati wa shambulio ilisikika milipuko na milio ya risasi katika eneo la hoteli hiyo na kwamba kuna milio mikubwa miwili isikika kwa kishindo kikubwa.


Kutokana na shambulio hilo la mlipuko inaelezwa watu kadha wamejeruhiwa ambapo maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu waliamua kutoa msaada kwa kushirikiana na watu wengine waliokuwa eneo hilo baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Mwandishi wa BBC ambaye yupo eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea mchana wa saa saba, Fredinand Omondi anaripoti kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa kikosi maalumu cha Recce squad kimewasili eneo la tukio ili kuongeza nguvu ya uokozi wa raia na kupambana na wavamizi.

Pia Omondi pia anaripoti kuwa moja ya maofisa usalama waliopo eneo la tukio amemwambia "hali sio nzuri". Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Kenya linaelezwa kuwa limeimarisha ulinzi eneo hilo huku wakiamua kuweka katazo la watu na magari kupita eneo ambalo limeshambuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...