Kama kuna mchezaji Mtanzania kwasasa mwenye kipaji cha kipekee na anaekubalika na wachezaji, wapenzi na viongozi wa SIMBA na YANGA basi ni AJIB.

Wazazi wa AJIB walifanya makosa kumzaa AJIB kipindi hiki. Huyu alipaswa kuzaliwa enzi za vipaji visivyo vya kawaida, enzi za MBWANA ABUSHIRI "Director", EMIL KONDO "Mzungu", JOHN LYIMO, SUNDAY MANARA "Computer", GIBSON SEMBULI, LEODGAR TENGA, ABDALLAH KIBADEN, KHALID ABEID, WILL MWAIJIBE, NICO NJOHOLE nk.

SIFA ZA AJIB:

1. Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa "kuupaka rangi mpira".

2. Ni mchezaji asiye na mpinzani kwenye mipira iliyokufa (Deadliest dead-ball specialist). 

3. Ni mchezaji mwenye kupiga krosi nzuri kuliko wote Ligi Kuu.

4. Ni mchezaji mwenye uwezo wa kufunga magoli ya kila aina.

5. Ni mchezaji asiye na uchoyo mwenye kupenda kusaidia wenzake wafunge .

6. Ni mchezaji mwenye assists nyingi kuliko wote katika Ligi Kuu (15).

7. Ni mchezaji aliyepewa TZS 3M msimu wa 2015/16 baada ya "kukokota kijiji" na kufunga goli la msimu.

8. AJIB msimu huu tu anazo FIVE goal of the season contanders!!

9. Tarehe 14.3. 2017, Zacharia Hanspope alimpatia TZS 200.000 mtoto aitwae AZIZ GASI kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma baada ya kujiandika jina AJIB mgongoni na Hanspope kukiri kuwa hata yeye anakunwa sana na maufundi ya Mtaalam AJIB.

10. HAJI MANARA, tarehe 19.4.2018, alisema "AJIB NI MZURI MARA TATU ZAIDI YA SAMATTA"
"AJIB anaanza vizuri sana msimu lakini akiishakuwa MFALME anapumzika. AJIB hapendi kabisa mazoezi. Kama angependa mazoezi, AJIB ni mzuri mara tatu zaidi ya MBWANA SAMATTA".
HAJI MANARA, 19.4.2018

11.  Wapenzi wa Yanga wanamkubali sana AJIB na jezi zake zinanunuliwa kama njugu na hata alipokosa penati jana alipigiwa makofi tofauti na ilivyokuwa MSUVA alipokuwa akikosa penati!!!.

AJIB,  kama binadamu mwingine,  ana udhaifu wake. Kama alivyosema HAJI, AJIB ni mvivu sana wa mazoezi. Lakini kwavile Yanga ina kocha bora sana, tatizo hilo linaonekanakupatiwa ufumbuzi. Kocha Zakhera amempa unahodha kitu ambacho kinamfanya kutobweteka na kuwajibika zaidi. HONGERA SANA MWINYI kwa uamuzi huo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...