Na Profesa Joseph Mbele
Mara moja moja, katika miaka kadhaa iliyopita, nimekuwa nikiwazia kufanya mpango wa kutafsiriwa kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kwa kiSomali. Niliwazia lugha hiyo kwa kuwafikiria waSomali waishio Marekani. Hapa kuna waSomali wengi kuliko sehemu yoyote duniani ukiachilia mbali Somalia yenyewe. Jimbo hili la Minnesota ninapoishi linaongoza kwa kuwa na waSomali wengi.

Nimekuwa na mahusiano ya miaka mingi na waSomali wa Minnesota, hasa katika miji ya Faribault na Minneapolis. Nimehusika katika kuwashauri kuhusu maisha ya hapa Marekani, mifano ikiwa ni mihadhara yangu Mankato na Faribault.

WaSomali ambao wamesoma kitabu changu wanakipenda sana na wananikumbusha tunapokutana. Mmoja wao ni rafiki yangu Mohamed Dini. Huyu ndiye tumekubaliana akitafsiri kitabu hicho. Yeye ni mmoja wa waSomali wachache sana wanaotambulika katika fani hiyo hapa Minnesota. Kazi hiyo itaanza mwezi huu.

Ni faraja kubwa kwangu kwamba tafsiri hii itakapochapishwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo yanayowakabili waSomali Marekani, ambayo ni mara dufu kuliko yanayowakabili waAfrika wengine wengi. Tofauti na waAfrika wengi, waSomali wengi hawajui kiIngereza ambayo ndio lugha ya Marekani. Vile vile, waSomali ni waIslam, dini ambayo ni ya wachache hapa Marekani, na sehemu nyingi hakuna yale ambayo waIslam wanahitaji kwa mujibu wa dini yao. Kuna juhudi zinafanyika, lakini bado hazijatosheleza.

Ninangojea kwa hamu maendeleo ya shughuli hii hadi ifikie lengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...