Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa Huduma bora.Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wataalamu wa Afya nchini kutambua kuwa wanatakiwa kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara. “Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini” alisema Makamu wa Rais.

Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto ni la ghorofa mbili na limegharimu jumla ya shilingi 3, 648,400,000/- na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Huduma zitakazopatikana kwenye jengo hilo la ghorofa mbili ni Huduma ya Mama na Mtoto, Wodi ya Wazazi na Watoto,Huduma ya Upasuaji kwa Mama Wajawazito, Huduma ya Vipimo X Ray, Utra Sound na Maabara, Ofisi za huduma za madaktari, wauguzi na wahudumu wengineo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongezi mara baada ya kukata utepe kuashiri uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Haji Omar Kheir (kulia) na kushoto ni Mkuu wa KMKM Komodoo Hassan Mussa Mzee
:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
 Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni, wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini Magharibi, Unguja ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...