Naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo akitoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha oktoba hadi desemba 2018 kwa baadhi ya waandishi wa habari mkoani humo. (picha na Mwamvua Mwinyi).

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Pwani, inaitilia shaka ujenzi wa miradi mikubwa mitatu ya afya na maji, yenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni 1.259 ambayo imeanza kuchunguzwa ili kubainika kama kuna ubadhilifu hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Aidha, imechukua hatua ya kuwahamisha vituo vya kazi askari wa usalama wapatao wanne baada ya kudaiwa kujihusisha na kuomba rushwa ,kwa kushirikiana na jeshi la polisi .

Akitoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha oktoba hadi desemba 2018 ,naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo alisema, jumla ya miradi Tisa iliyogharimu Bilioni 3.373 .670 ilifuatiliwa katika kipindi hicho.

Hata hivyo alieleza, miradi hiyo ni pamoja na sekta ya maji, afya, uvuvi na elimu, kati ya miradi hiyo mitatu inadaiwa kuwa na ubabaishaji.

Alitaja mikakati waliojiwekea kwa mwaka 2019 ikiwemo kufuatilia miradi ya maendeleo inayoendelea katika halmashauri mbalimbali ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa kiwango kinachotakiwa.

Nombo alisema, watakaa na wadau kwa yale maeneo waliyoyabaini yana mianya ya rushwa na kuweka mikakati ya kuziba mianya hiyo.

Pia wataendelea kufanya uchunguzi kwa zile taarifa ambazo tayari wamezipokea na hasa za rushwa ndogo ambazo ni kero kubwa ndani ya jamii.

"Uchunguzi utakapobainika pasipo shaka kuwa kuna yeyote aliyejihusisha rushwa atafikishwa mahakamani "alisema Nombo.

Akizungumzia rushwa ya barabarani Nombo aliwaasa, wamiliki wa magari mbalimbali kutengeneza magari yao na kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na mkono wa askari wa usalama barabarani.

Alitoa rai kwa madereva endapo wakiombwa rushwa na askari wa usalama barabarani wanapaswa kupiga simu namba 113 ili mhusika achukuliwe hatua stahiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...