Baadhi ya Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji cha Lositete wakiingia kwenye gari la polisi kuelekea kituo cha polisi Karatu kuandika maelezo ya kwanini wanashawishi wananchi kugomea shughuli za maendeleo. Agizo hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo


Na.Vero Ignatus, Karatu


Wito umetolewa kwa wazazi pamoja na walezi wilayani Karatu kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule hata kama hawana sare za shule.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika kijiji cha Lositete Kata ya Mbulumbulu Wilayani Karatu wakati alipokwenda kukagua hali halisi ya madarasa pamoja na wanafunzi wangapi wameshaanza masomo ya kuanza kidato cha kwanza.

Gambo ameuagiza uongozi wa serikali ya kijiji cha Lositete kuchukuliwa maelezo polisi ni kwanini hawachangii maendeleo ya elimu badala yake kuingiza siasa na kusababisha saruji kuganda pamoja na mifuko 71 ya saruji, mbao kuoza kwa kipindi cha miaka miwili.

Yote hayo yamekuja mara baada yakushtushwa na taarifa aliyoitoa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Upper Kitete, Josephat Mau iliyodai kuwa wanafunzi tisa kati ya 171 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo hawajaripoti shuleni kutokana na kukosekana kwa sare za shule.

Mwalimu Mau alisema wanafunzi hao 9 hawajaripoti shuleni hapo kutokana na kukosekana na sare za shule huku walioripoti wakiwa ni tisa tu kwasababu ya wazazi au walezi wao kutouza maharage kutokana na kukosekana kwa soko.

Baada ya Mwalimu huyo kutoa taarifa hiyo ndipo Rc Gambo aliagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni na nguo za nyumbani hata kama hawana sare ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakisubiri kuwanunnulia mahitaji ya shule.

"Rais ameagiza elimu bure hivyo wazazi au walezi watoeni watoto wenu majumbani ili waende shule bila ya kuwa na sare za shule huku mkiendelea kutafuta sare lakini pia nasisitiza nyie wananchi acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo na wewe nyie viongozi wa vijiji pamoja na kata muwe na tabia ya kusoma mapato na matumizi ya vijiji "Alisema Gambo

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete Rc Gambo aliagiza mwenyekiti wa kijiji cha Upper Kitete, William Safari pamoja na William Marmo kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wanadai hawajasomewa tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2018.

Awali baadhi ya wananchi hao, Pascal Paulo na Kastuli Dizderi walidai kuwa wameshindwa kujenga madarasa pamoja na maabara kwasababu walichanga fedha ambazo zililiwa na aliyekuwa Mkuu wa shule hiyo wa zamani Andrew Sulle ambaye alichukua sh, milioni 8 walizochanga kwaajili ya ujenzi wa madarasa na maabara kuliwa na aliyekuwa mwalimu mkuu wa zamani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo alisema wananchi zaidi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete wanapenda kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo na amejitahidi kutatua changamoto zao ikiwemo kuhakikisha Mwalimu Mkuu huyo wa zamani Sulle anachukuliwa hatua za kinidhamu na ameshahukumiwa kifungo.

Alisema wanafunzi 5,313 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana huku wanafunzi 4,000 sawa na asilimia 75.3 walifaulu ambapo wanafunzi 3,446 wakiwa wamepangwa kwenye shule za kata zilizokuwa na madarasa 83 na wanafunzi 539 walikosa nafasi.

Alisisitiza kuwa wanafunzi hao 539 waliokosa nafasi hivi sasa wameshaanza masomo katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kutokana na kubainika kunashule wanafunzi hawkaupangwa kabisa huku wakiandika barua kw wadau nakuhamasisha wanananchi kujenga madarasa pamoja na kikarabati viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...