Na Jeshi la Polisi
Timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania bara imesema mwaka huu ni mwaka wao wa kuhakikisha kuwa wanafanyaa vizuri ili kupanda na kucheza ligi kuu Tanzania.
Akizungumza na gazeti hili Afisa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Frank Lukwaro amesema msimu huu wamejipanga ikiwemo kuwashirikisha wadau muhimu katika kuleta mafanikio ya ushindi hususani katika mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki huku timu hiyo ikiwakaribisha wababe wa Simba timu ya Mashujaa kutoka Kigoma.
Lukwaro amesema mashabiki wa mkoa wa Kilimanjaro hivi sasa wameungana pamoja katika kuhakikisha kuwa timu inapata ushindi katika kila mechi iliyosalia ili kujiweka katika nafasi za juu katika kundi B.
Amesema pamoja na kujitokeza kwa wingi uwanjani lakini pia wamekuwa wakitoa ushauri wa nini cha kufanya  kwa ushirikiano wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro KRFA na wafadhili wa timu hiyo kampuni ya Lodhia na Busega Mazao.
‘Hivi sasa timu yetu inacheza vizuri kulingana na usajili makini walioufanya katika dirisha dogo na mwalimu Mbwana Makata ameimarisha kikosi chake vilivyo ndio maana uwanja sasa unajaa mashabiki na hamasa ni kubwa tofauti na hapo awali’ Alisema Lukwaro. Kwa upande wake kocha Mbwana Makata akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Mashujaa amesema kikosi chake kipo imara na ana imani kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Makata amesema kila mechi katika mzunguko wa pili anaipa umuhimu mkubwa hivyo amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kujituma na kufuata maelekezo aliyowapa ili kuibuka na ushindi.
Mpaka sasa timu hiyo ipo nafasi ya saba katika msimamo wa kundi B ikiwa imejikusanyia alama 14 katika michezo 11 baada ya kushinda michezo mitatu, kutoka suluhu michezo mitano na kupoteza michezo mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...