*Aagiza zipigwe rangi zisafirishe Watanzania...asema kwanza yeye hasafiri sana

*Azungumza mambo makubwa kuhusu Watanzania, Balozi wa Canada aacha somo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza ndege za Rais mbili zipigwe rangi ya Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) ili zitoe huduma ya kusafirisha Watanzania kati ya eneo moja na jingine.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza baada ya kupokea ndege mpya ya Airbus 220-300 iliyowasili leo Januari 11 ,2018 ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uamuzi wake wa ndege mbili za Rais zitumiwe na Shirika la Ndege.

Amefafanua kuwa ndege ambazo zimetengwa kwa ajili ya Rais zipo tatu na hivyo ndege mbili amezitoa ili zitumike kutoa huduma."Kwanza Rais mwenyewe sisafiri ,hivyo ndege hizo zipigwe rangi ya ATCL zitoe huduma ya kwenda mikoa mbalimbali nchini,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli amesema Shirika la Ndege la Air Tanzania kwa asilimia 100 linamilikiwa na Watanzania wenye na hilo ni jambo la kujivunia sana na hayo ndio matokeo ya kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo.

Amesema kuna mashirika makubwa ya ndege ambayo yameandikwa majina ya nchi zao lakini si za nchi hizo lakini kwa ndege za ATCL ni mali ya Watanzania huku akifafanua ndege hizo ni za Serikali kwa asilimia 100.

Amesema Tanzania tunaweza na moyo wa kizalendo wa Watanzania upo ukiondoa wachache ambao hawana uzalendo na hao hawakosekani."Niwaahidi kwa nguvu zangu zote na ajili zangu zote niwatumikie Watanzania.

"Namuomba Mungu nisiwe na kiburi na majivuno.Namuomba Mungu aniongeze mimi na Serikali tuwatumikie Watanzania na hasa wanyonge bila kujivuna," amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Bunge ambalo limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali na kwamba hata walipoamua kupitisha bajeti ya ununuzi wa ndege hizo ilitokana na uzalendo wao.

"Nawapongeza wabunge wote na haswaaa wabunge wa CCM ambao linapokuja suala la maendeleo wanaitikia ndiooo," amesema Rais Magufuli huku akisisitiza upendo na mshikamano kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Akizungumzia ndege hizo amesema miaka ya nyuma ndege kubwa zilikuwa zipo kwa nchi nyingine lakini leo hii zipo Tanzania na ndege ambazo zimebunuliwa za Airbus zipo nchi kwetu tu na hazipo mahali popote Afrika.

Amesema kuwa Tanzania itakuwa kama Ulaya na amewataka Watanzania kuamini kwenye hilo na kwamba ukiwa na imani unafanikiwa na hivyo Watanzania watafanikiwa sana.Amesema Tanzania ambayo anaitaka yeye ni ile ambayo huduma mbalimbali za kijamii ziwe zimeboreshwa na kwamba anaamini ndege zitaendelea kuongezeka.

Amesema Tanzania mpya inakuja na wanaochonganisha washindwe kwa la Yesu na Mtume Muhhamad huku akifafanua dua ambazo zimeombwa na viongozi wa dini Mungu amesisikia.

Ametumia nafasi hiyo kuwaombea Watanzania wote wafanikiwe kwenye mambo yao mbalimbali.Wakati huo huo Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kumpongeza Balozi wa Canada nchini Tanzania kwa uamuzi wake wa kuzungumza Kiswahili na amewafundisha Watanzania umuhimu wa kuzungumza Kiswahili.

Amesema kuna Watanzania ambao wamekuwa wakizungumza Kingereza na kujiona ni ufahari ambapo wanashindwa kuwafundisha lugha ya makabila ya Tanzania."Balozi na kupongeza na wale Watanzania wanaona 
aibu kuzungumza Kiswahili uwe mwalimu wao."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...