Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya tamasha la Sauti za Busara kuanza, Mwenyekiti wa Busara Promotions Simai Mohammed Said amewataka watanzania na wakaazi wa Zanzibar kwa ujumla kuchangamkia fursa zinazo tokana na tamasha hilo. 

“Kuna offa maalum kwa ajili ya watanzania ambayo ni ya chini kabisa ukilinganisha na kile wanacholipa wageni kutoka sehemu zingine kuingia kwenye tamasha,” alisema Simai. 

Alisema fursa zinazo tokana tamasha hili haipatikani mahali popote na wanaofaidika zaidi ni wakazi wa mitaa ambao bado wanashindwa kutumia hizo fursa kikamilifu . 

"Kuna nyakati ambazo watu wanauliza maswali mengi kuhusu tamasha laSauti za Busara na wengine wanakwenda mbali hadi kusema kuwa ni tamasha kwa watalii wakati wao ndio wenyeji," alisema Bw Simai .Mwenyekiti wa Bodi zaidi aliongeza: 'Hakika hakuna haja ya kuangalia mbali sana kupata majibu ya maswali kama hayo; Kwa miaka 16 iliyopita muda huu umekuwa msimu wa juu kwa biashara ya utalii kulingana idadi ya wageni wanaokuja Zanzibar’. 

Kulingana na yeye kuna dalili kwamba hoteli zote za Zanzibar zimejaa kikamilifu na Jiji la Zanzibar kwa ujumla ipo katika hali ya matarajio.Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobsen kwa upande wake atakuwa akihudhuria tamasha kwa mara ya kwanza na anatarajia mengi kutoka kwenye tamasha hilo hususan fursa zinazopatikana kwenye tamasha. 

“Tunaendelea kusaidia shughuli za kitamaduni kama Sauti za Busara kwa sababu tunaelewa thamani ya shughuli hizo. Tunaona hii ni jukwaa muhimu la kujieleza bure, kukuza tamaduni zetu, weledi na utaalamu katika sekta ya kitamaduni ya Tanzania "alisema Balozi huyo wa Norway, ambaye alianza majikumu yake la kidiplomasia mnamo Septemba 2018. 

Pia aliwahimiza wafanyabiashara ambao ni walengwa wakuu wa tamasha kuunga mkono tukio hilo kwa namna ya uwajibikaji kwa jamii.Julia Bishop ambaye ni makamu wa Mwenyekiti kwa upande wake alisema amejionea mwenyewe jinsi tamansha la Sauti za Busara linavyo badilisha maisha ya wasanii hususan wale chipukizi wasiojulikana kabisa. 

“Kwa mtu ambaye hajawahi kufika Zanzibar kabla ni vigumu kufikiria ukubwa wa tukio hili, ubora wa maonyesho, utaalamu na msisimko ambayo hupatikana ndani ya Stone Town, "alisema.Kulingana na yeye, ukweli kwamba makundi madogo ambayo haijulikani sana kupata fursa sawa na nyota wa muziki kwenye jukwa moja yenyewe ni hatua ya kubadili maisha. 

Tamasha la Sauti za Busara linadhaminiwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Ujerumani, Pro Helvetia, Zanlink, Mozeti, Shirika la Ndege la Ethiopia, African Movie Channel, Zanzibar Media Corporation, TV-E, E-FM, Madinat Al Bahaar, Golden Tulip na wengine wengi. 

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la Kiafrika linalofanyika kila mwaka, mwezi Februari mjini Zanzibar, Tanzania katika eneo la Ngome Kongwe (Old Fort) sambamba na matukio mengine ya kuvutia yanayofanyika kwa wakati mmoja maeneo ya Stone Town- ikiwemo Carnival Street Parade, Swahili Encounters, Movers & Shakers na Busara Xtra. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...