Tamthilia kali ya Wildflower inarudi tena kwenye king’amuzi cha StarTimes. Msimu wa pili wa tamthilia hiyo ya kifilipino utaanza kuonekana Usiku wa Januari 20 mwaka huu kupitia ST Novela E Plus pekee. 

Wildflower ni miongoni mwa tamthilia zilizofanya vizuri zaidi nchini Ufilipino katika mauzo pamoja na kupokelewa vizuri na watazamaji na pia Msimu wake wa kwanza ulifanya vizuri sana kwa nchi za Afrika mwaka jana.

“Tulifahamu kwamba Wildflower ni tamthilia nzuri ila hatukujua kwamba ingefanya vizuri kuliko tamthilia zote. Mashabiki na wafatiliaji wa tamthilia hii wamekuwa wakiulizia msimu wa pili tangu msimu wa kwanza ulipoisha”. Zamaradi Nzowa,  Meneja Maudhui StarTimes. “Tunafurahi sana kuanza mwaka 2019 kwa kuwaletea tamthiliya hii, niamini napokwambia, kama uliupenda Msimu wa kwanza basi huu wa pili ni kiboko zaidi”. Aliongeza.

Muhusika mkuu kwenye tamthiliya, Maja Salvador anashukuru tamthilia hiyo kupokelewa vizuri na watazamaji. “Tungependa kuwashukuru watazamaji wetu kwa upendo na kuipokea vizuri tamthiliya yetu kwa msimu wa kwanza. Msimu huu wa pili tunawaahidi mambo makubwa na visa mbalimbali. Tuna imani mtaendelea kutuunga mkono,” Maja alisema kwenye mahojiano.

Tamthiliya ya Wilflower inatengenezwa na ABS-CBN, ni kisa kinachomuhusu mwanamke mwenye Ujasiri, malengo na ustahimilivu wa kutafuta haki kwa ajili ya familia yake na watu wa mji wake. Akisukumwa na upendo na matumaini, mhusika mkuu Lily/Ivy anapigania kile anachokiamini bila kujichukulia sheria mkononi.

Mambo yatakuwa magumu kadri mvutano unavyozidi kuongezeka. Kufuatia kifo cha Nay Carlota, Ivy anazidi kushawishika kuwaangusha familia ya Ardiente. Ivy atafanya nini kupata haki ya Carlota? Hakuna cha kumzuia Diego kugombea ugavana wa Poblacion Ardiente dhidi ya kaka yake, Arnaldo. Je atashinda au atazungukwa na familia yake? Kwenye mapenzi, Arnaldo ataangukia mtego wa Ivy? Je Diego ataweza kutenganisha hisia zake kwa Ivy na wito wake?
Majibu ya maswali yote haya yapo ST Novela E Plus Ijumaa hadi Jumapili saa 2:50 Usiku, sehemu mbili kila siku kuanzia tarehe 20 Januari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...