Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA
la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Arusha limesema kwa kushirikiana na
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jery Murro wamefanikiwa kudhibiti vishoka na
wahujumu wa miundombinu ya shirika hilo.
Hayo
yameelezwa na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina
wakati anazungumzia hatua ambazo zimefanyika katika kukabiliana na
vishoka pamoja na wahujumu wa miundombinu.
Kuhusu
vishoka amesema TANESCO wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali
kukabiliana na vishoka na baadhi ya hatua hizo kwa wale ambao
wanabainika wanachukuliwa hatua.Pia wamekiwa wakiondoa miundombinu ya
umeme ambayo imewekwa na vishoka.
"Maeneo
ya USA tuling'oa nguzo ambazo ziliwekwa na vishoka,pia tumekuwa
tukiondoa hata LUKU ambazo tunabaini zimewekwa na hao vishoka.Tumechukua
mbalimbali ikiwamo ya wanaobainika kuchukuliwa hatua ya kupelekwa
Polisi sheria ichukue mkondo wake.Tumefanikiwa sana kuwadhibiti vishoka
kwani TANESCO tupo makini .
"
Tunashirikiana kwa karibu na Mkuu wa Wilaya Murro,kila tunapomueleza
katika hili anatoa ushirikiana na kwenye matukio mengi yanayohusu
kukamata vishoka au wanaohujumu miundombinu amekuwa pamoja
nasi,"amefafanua Mhandisi Mhina.
Kwanini
Murro amekuwa akishiriki kwa karibu kukomesha vishoka,Meneja Mhina
amejibu kuwa katika Wilaya ya Arumeru tatizo la vishoka na wanaohujumu
moundombinu lilikuwa kubwa na katika kulishughulikia walimpa taarifa
Mkuu huyo wa Wilaya na tangu alipofika wanashirikiana sana.
Ameongeza
katika hujuma ya miundomboni nayo wamefanikiwa na wanaendelea
kufuatilia hatua kwa hatua ili kuwabaini wenye kuiharibu
miundomboni."Kuna watu wanaiba waya wa mita 10,sasa hiyo ni hujuma ya
miundombinu ya umeme."
Kwa
upande wake Menaja Mwandamizi wa Miradi TANESCO Mhandisi Emmanuel
Manirabona amezungumzia mikakati ya shirika hilo la kudhibiti vishoka
ambapo amefafanua moja ya mkakati ni kuhakikisha vifaa vyote vya shirika
hilo vinabaki kuwa mali ya shirika.
Amesema
hivyo hata mfanyakazi au mtumishi yoyote wa TANESCO ataruhusiwa kutumia
mali ya shirika hilo akiwa mfanyakazi na baada ya hapo hataruhusiwa.
"Ukifuatilia
utaona matangazo pale inapotokea kuna mfanyakazi wetu ameondolewa
TANESCO na wakati mwingine tunasema kuwa mtu fulani si mfanyakazi wetu
na hatutahusika na chochote ambacho atakifanya,"amesema Mhandisi
Manirabona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...