Naibu waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani Mh. Jumaa Aweso amewataka wahandisi wasiokuwa na sifa na Vigezo ndani ya wizara hiyo hususani wahandisi wababaishaji, kujitathimini mapema kwani msasa utapita kwa ajili yao.

Naibu waziri Aweso ametoa tamko hilo akiwa Mkoani Kagera katika ziara Mahsusi iliyoanzia katika Ofisi za Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mjini Bukoba (BUWASA), kisha kutembelea kituo cha uzalishaji maji kilichopo Bunena, Bukoba Manispaa na baadae kukagua tanki la Maji lililopo Kashura na lile linalojengwa Ihungo ndani ya Manispaa.

Katika ziara hiyo akiambatana na Mstahiki Meya Chief Kalumuna, Mkurugenzi wa maji (BUWASA), wahandisi na wataalamu wa Idara hiyo, Naibu Waziri Amefurahishwa na Kukamilika kwa Mradi huo wa Maji mjini Bukoba uliogharimu zaidi ya shilingi. Wenye uwezo wa kuzalisha lita za maji zaidi ya Milioni 18 wakati mahita ji wa wakazi wa manispaa ya Bukoba ni lita Milioni 13.

Licha ya kukamilika kwa mradi huo kuna baadhi ya maeneo hawajafikiwa na huduma hiyo muhimu ya maji, bado Maeneo ambayo mpaka sasa hayajafikiwa na mradi nayo ni pamoja na Buhembe, Nyanga Nshambya Kahororo Ijuganyondo na Kibeta, na Hivyo kumuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji kushughulikia suala hilo kwa karibu ili kufikia malengo yaliyowekwa ambayo ni kila mwananchi kupata Huduma ya maji safi na salama.

Sambamba na hayo Wananchi wametakiwa kuendelea kutunza na kulinda vyanzo vya maji ikiwemo miundo mbinu ya maji ili iendelee kuwanufaisha katika maisha ya kila siku, ambapo asilimia kubwa hutegemea maji kwa matumizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kulipia Ankara zao za maji pasipo kususbiri hadi kukatiwa huduma.

Mh. Awesso yupo Mkoani kagera katika ziara ya kikazi na anategemea kutembelea wilaya zote akiwa tayari amehitimisha ziara yake Bukoba Manispaa.
 Moja kati ya Matanki ya Mradi wa maji yanayoendelea kujengwa ndani ya Manispaa ya Bukoba unavyoenekana mara baada ya Mh. Aweso kuutembelea.
 Pichani Mh. Jumaa Aweso Naibu Waziri wa Maji, akiteremka kwenye ngazi za Tanki lililopo Ihungo Manispaa ya Bukoba, mara baada ya kulidhishwa na shughuli ya Ujenzi Inayoendelea.
 Mh. Aweso pamoja na Uongozi wa BUWASA wakimsikiliza Mstahiki meya Mh. Kalumuna wakati akizungumza katika kikao cha Viongozi na Naibu Waziri.
 Pichani ni msafara wa Mh. waziri pamoja na Wataalamu wakikagua moja kati ya vituo vya maji vilivyopo Bunena, ambapo maji lazima kupitia kabla ya kusambazwa kwa matumizi ya Nyumbani.
Pichani Mh. Jumaa Aweso Naibu Waziri wa Maji, akiteremka kwenye ngazi za Tanki lililopo Ihungo Manispaa ya Bukoba, mara baada ya kulidhishwa na shughuli ya Ujenzi Inayoendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...