NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MKUU wa Mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wananchi waliovamia eneo lenye ukubwa wa hekari 500 ,Pangani huko Kibaha na kujigawia viwanja waondoke mara moja .

Aidha amelitaka jeshi la polisi kumkamata mtu yoyote atakayekutwa kwenye eneo hilo na wale waliouziwa kwenda polisi ili wahusika ambao ni matapeli waweze kukamatwa kwani eneo hilo linamilikiwa kihalali.

Ndikilo aliyasema hayo alipotembelea eneo hilo ambalo linamilikiwa na mtu anayefahamika kwa jina la Seamens na maeneo mengine yenye ukubwa wa hekari 500 yanayomilikiwa na watu wengine wawili ambao hawajaendeleza kwa kipindi kirefu hivyo wananchi kuamua kujigawia viwanja kinyume na taratibu. 

Alieleza, wananchi hao wanapaswa waondoke ili halmashauri ifanye utaratibu wa kulirudisha eneo hilo serikalini baada ya mmiliki wake kushindwa kuliendeleza na kuwa pori, na sehemu ambayo watu wanauwa na kutupwa .

"Kuna watu 18 ambao wanajifanya ndiyo viongozi na wamewagawia watu maeneo, hatua 30 kwa 30 kwa kila mtu na eneo hilo wahalifu wamelifanya eneo hilo kwa ajili ya kupumzikia baada ya kufanya uhalifu au wanapowateka watu au kuwaua"alifafanua.

“Tunajua kuna mahitaji makubwa ya ardhi lakini si kwa utaratibu huu mchakato unaendelea tutapeleka mapendekezo kwa waziri wa ardhi nyumba na makazi naye atapeleka kwa Rais kwa ajili ya kufuta umiliki kisha Halmashauri litapanga utaratibu na kuwagawia wananchi kutegemeana na mahitaji ya viwanja na mipango miji ,” alibainisha Ndikilo.

Aliitaka hiyo kamati iliyounda na kuwauzia watu wawarudishie fedha wale waliowauzia kwani wamewatapeli na serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hilo kwani mara baada ya kurudi litapangiwa utaratibu kwani kwa sasa mji huo unapangwa ili kuelekea kuwa Manispaa 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alisema kuwa wananchi hao kutoka maeneo mbalimbali ya Kibaha na Dar es Salam waligawana maeneo hayo ambayo yanamilikiwa na watu watatu.

Alieleza, mtu wa kwanza eneo lake lina ukubwa wa hekari 300 ,mwingine 200 na wa tatu 500 ambapo wananchi waliamua kugawana viwanja kinyume cha sheria .Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka alisema eneo hilo lina wamiliki hivyo ni vema kukaa nao na kuangalia mipango miji ya serikali katika kuupanga mji wa Kibaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...