Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania Mhe. Mhe.Gullam Hafeez Mukadam akiwa na Katibu Mkuu wa ALAT Abdallah S. Ngodu wakielezea kuhusu Tuzo za Meya.

Mratibu wa Mradi wa Tuzo za Meya Wilman Ndile(kulia) akizungumza namna Tuzo za Meya zitakavyoshindanishwa kwa Halmashauri zote Tanzania. 
 
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu ALAT Taifa Abdallah S. Ngodu, Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Gullam Hafeez Mukadam, Makamu Mwenyekiti Stephene Mhapa akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Maboga Iringa Dc Mhe Veny Muyinga wakati wa utambulisho wa Tuzo ya Meya kwa mwaka 2019.

……………………………………………………………………………….
 

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) imehuisha Tuzo ya Meya na kwa mara nyingine tena zitafanyika kuanzia Mwaka huu 2019, ambapo Halmashauri zote nchini zitashindanishwa kupata halmashauri moja katika kila kipengele na hatimaye kupatikana Halmauri yenye kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Akizungumza jijini hapa, Mratibu wa Tuzo ya Meya toka ALAT, Wilman Ndile alisema uzinduzi wa tuzo hiyo unatarajia kufanyika Juni mwaka huu katika jiji la Mwanza.

Alisema tuzo hiyo inalenga kuibua ari na ushindani katika kuwahudumia wananchi na zaidi kuwafanya viongozi na watendaji wa Halmashauri zote kujituma na kubuni miradi itakayowaongezea mapato huku wakimuwezesha mwananchi kutumia njia bora kujiletea maendeleo..

Ndile alisema mchakato wa uteuzi katika mashindano utahusisha umma wa watanzania ambao watatuma ujumbe mfupi kuchagua halmashauri bora, na kuongeza kwamba majaji watatembelea halmashauri husika kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuchagua manispaa bora.

Ndile aliongeza kuwa maombi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho yatahusisha ujazaji wa fomu ambazo kwa wakati huu fomu hizo ni rafiki na unaweza kuzijaza hata kwa njia ya mtandaoni na si zile za kuandika kwa mkono kama ilivyokua hapo awali hivyo halmashauri zote zitajulishwa na kutumiwa fomu hizo kwa njia ya posta lakini pia kwa barua pepe na wao watachagua njia rahisi kwao katika ujazaji wa fomu hizo.

“Baadhi vipengele ambavyo vitashindwanishwa ni kama vile Halmashauri iliyofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, Halmashauri iliyoleta uvumbuzi na teknolojia katika utoaji wa huduma pamoja na Halmashauri iliyotekeleza miradi kwa ubora unaotakiwa” alisema Ndile.

Vipengele vingine ni pamoja na Halmashauri iliyotoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa mujibu ya mapato yao, Halmashauri iliyowajengewa wananchi uwezo wa kujikwamua kiuchumi, na Halmashauri inayofanya vizuri katika Utawala bora.

Tuzo hizi zilzoanzishwa Mwaka 2015 zimejikita katika kutunza utendaji kazi bora na jitihada zisizo za kawaida, ugunduzi, moyo wa kujitolea na utayari unaozidi kiwango cha kawaida kinachotarajiwa kwenye kazi za halmashauri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...