NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

WAZAZI na walezi walio na watoto wenye ulemavu ,wameaswa kuwafichua watoto wao walio na sifa ya kuanza elimu ya awali badala ya kuwaficha na kusababisha kukosa haki ya kupata elimu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujifunzia, kusomea na vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule za awali mkoani Pwani ,vilivyogharimu milioni 48.5 kutoka shirika la kimataifa la ADD, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, aliomba jamii ihamasike na kuibua watoto hao.

Alieleza ,endapo tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu itaachwa itasaidia kupunguza idadi kubwa ya watoto walio na ulemavu mbalimbali ambao hawajaandikishwa shule.

“Watoto wenye ulemavu wapelekwe shule kama wasio na ulemavu kwani wote wana haki ya msingi kupata elimu kuanzia awali hadi chuo kikuu “alisisitiza Assumpter. 

Aidha Assumpter aliitaka jamii, kufuatilia na kuwakemea watoto wanapokosea ama kugundua wanajiingiza kwenye makundi yasiyo na maadili, ikiwezekana wachapwe viboko ilihali kuondokana na wimbi la watoto Dotcom

Awali ofisa program uhamasishaji wa shirika la kimataifa linalotetea na kuhudumia watu wenye ulemavu nchini (ADD)Isack Idama alisema, wametoa vifaa hivyo vilivyogharimu milioni 48.5 ambapo vitagawiwa katika shule tano kwenye kila halmashauri mkoani hapo. 

Alifafanua kwamba, mgao huo ni awamu ya kwanza hivyo wanatarajia kutoa vifaa vingine hivi karibuni katika shule nyingine ishirini .

Alieleza, wanatekeleza miradi ya elimu jumuishi kwa kufanyakazi na wizara ya elimu na TAMISEMI kuboresha elimu na mradi unatekelezwa hadi mwaka-2021,ambapo hadi sass watoto 395 wameandikishwa shule za awali tangu mradi uanze.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...