Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Msuguri, nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amekutana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Msuguri, nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Jenerali Msuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya mwaka 1980 hadi 1988 wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Serikali ya Awamu ya Pili ya Mhe. Ali Hassan Mwinyi.

Jenerali Msuguri alikuwa mstari wa mbele katika kupigana vita dhidi ya Nduli Idd Amin ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilivyopigana kuukomboa Mkoa wa Kagera wakati Iddi Amin alipovamia Novemba 1978.

Jenerali Msuguri ndio mwanzilishi wa eneo maarufu lililopo jiji Dar es salaam lijulikanalo kama Mbezi kwa Musuguri, ambapo aliishi wakati akiwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania.

Dkt. Mabula amekutana na Jenerali Msuguri wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara ambapo katika maongezi yao Jenerali Msuguri alimgusia kuhusiana na uvamizi unaosemekana umefanywa na wakazi wanaozunguka eneo lake lililopo Kimara Temboni, jijini Dar es salaam lenye Hati namba 231.

Katika eneo hilo lenye ekari 17 Jenerali Msuguri amemueleza Dkt. Mabula kwamba inasemekana tayari ekari 3 zimeishavamiwa na baadhi ya wakazi ambao wanalima na baadhi wamejenga makazi yao huku wakigoma kutoka kwa kutumia nguvu.

Miongoni mwa watoto wa Jenerali Msuguri Bi. Felista Musuguri alimueleza Dkt. Mabula kwamba walifanya jitihada za kuwaondoa watu wanaosemekana ni wavamizi lakini walikimbizwa na mapanga hivyo wanaogopa isije ikatokea machafuko.

Kwa sasa Jenerali Msuguri yupo nyumbani kwake katika Kitongoji cha Kitanga, Wilaya ya Butiama mkoani Mara jirani kabisa na Kijiji cha Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo.

Akiwa Wilaya ya Butiama Dkt. Mabula alifika katika Kijiji cha Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo na kuzuru Kabuli la marehemu Julius Nyerere, Mkoa wa Mara.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Musuguri (katikati) akimuonesha wanafamilia wake Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi na wanafamilia wengine.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali David Musuguri (nguo nyeupe katikati) akiwa na wanafamilia wake, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi na wanafamilia wengine.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akisali katika kabuli la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara wakati alipofika kuzuru Kabuli hilo.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwasha mshumaa katika kabuli la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara wakati alipofika kuzuru Kabuli hilo.
Naibu Waziri, wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwa Nyumbani kwa Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo Mkoa wa Mara, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...