*Asema wasipofurahia treni ya umeme,mnataka wafurahie ya dizeli?

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MSANII maarufu nchini Peter Msechu amesema anashangazwa na moyo wa choyo walionao baadhi ya Watanzania ambao kwao ni ngumu kupongeza juhudi za Serikali na badala yake kazi yao ni kutukana wale wanaoamua kutembelea miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Msechu ametoa kauli hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro akitokea Dar es Salaam kwa usafiri wa treni yeye pamoja na wasanii wengine wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Wasanii wa fani mbalimbali nchini leo Februari 7,2019 wamepata fursa ya kutembelea ujenzi wa reli ya treni ya kisasa ambayo itatumia umeme ambapo Msechu amepongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa fedha za ndani.

"Tumefurahi kuwa sehemu ya Watanzania ambao tuliobahatika kuutembelea ujenzi huu wa reli ya kisasa.Ila inasikitisha sana tunapoonekana kwenye miradi mikubwa kama hii ambayo ina tija kwa Taifa letu baadhi ya watu wanatutukana na kusema tumenunuliwa," amesema Msechu.

Ameongeza kuwa ingekuwa leo Makonda angeamua kuwachukua wasanii wa Kenya na Uganda anaamini Watanzania wangelalamika kwanini wamechukuliwa wasanii wa Tanzania hawakuchukuliwa kwenda kuona utekelezaji wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.

"Leo Mkuu wa Mkoa kaamua kutuchukua sisi tuambatane naye msema....mnataka mtuone wapi?Mara ooh mmelipwa sasa sisi kazi yetu nini.Kwani tukilipwa na sisi tukalika kodi Serikalini kuna tatizo gani?

" Mnataka kutuambia huu mradi wa reli ya kisasa hauna manufaa kwa Watanzania wakati kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika Serikali haiboreshi reli ya kati,leo hii inaboreshwa mnataka tubeze,"amesema Msechu.

Ameongeza msanii huyo kuwa "Serikali hii ni yangu,Rais Magufuli huyu ni wangu ,kodi nalipa kwa fedha yangu,mazuri nitayasema kwa nguvu zangu zote.Niache kufurahia treni ya umeme nifurahie treni ya dizel?Hata mwehu atanicheka."

MSANII maarufu nchini Peter Msechu akiwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...