Bondia namba moja wa uzito wa Super Welterweight, Hassan Mwakinyo na bondia nyota wa kike nchini Kenya, Fatuma Zarika wamewasili mjini Liverpool kujiandaa na pambano la ngumi za kulipwa mjini Nairobi, Kenya mwezi ujao.

Mwakinyo na Zarika ambapo wapo chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, watapambana na mabondia tofauti katika pambano lililopewa jina la Nairobi Fight Night katika ukumbi ambao utatangazwa hapo baadaye.

Mwakinyo ambaye bondia namba 16 kati ya mabondia 1,842 kwa mujibu wa viwango vya mtandao maarufu wa ngumi za kulipwa Duniani, Boxrec, Bondia huyo mzawa wa mkoa wa Tanga,  kwa sasa ana rekodi ya kushinda mapambano 24, kati ya hayo, 10 kwa knockout (KO) na kupoteza mawaili ikiwa moja kwa KO.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema kuwa mabondia hao wawili watakuwa chini ya kocha wa bondia  nyota, Tony Bellew ambaye alimchapa kwa TKO mara mbili, bondia maarufu, David Haye.

Abbas alisema kuwa Mwakinyo na Zarika watarejea moja kwa moja nchini Kenya Machi 16 tayari kwa mapambano yao. Zarika ambaye ni maarufu kwa jina la “Irone Fist”  atatetea ubingwa wake wa Baraza la Ngumi za Kulipwa (WBC) wa uzito wa Super Bantamweight, atapambana na bondia nyota kutoka Zambia, Catherine Phiri. 

“Lengo la kuwatafutia kambi ya mazoezi nchini Uingereza ni kuwaboresha ukali wao ili waendelee kutamba katika mchezo wa ngumi za kulipwa Duniani. SportPesa inajivunia kuwa na mabondia hawa na tunaamini hawatatuangusha katika mapambano yao,” alisema Abbas.

Abbas aliwaomba mashabiki wa ngumi za kulipwa kufika kwa wingi wakati wa mapambano hayo ili kuwapa hamasa mabondia hao ambao ni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Mwakinyo aliishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuwatafutia kambi ya mazoezi, jambo ambalo  hakuwa anafanya kabla ya kupata umaarufu.

“Ni faraja kwangu na mchezo wa ngumi za kulipwa pia. Naamini mabondia wengine wataongeza bidii ili kuweza kufikia kiwango change na kupata wadhamini kama SportPesa ambao wamenyesha njia kwangu,” alisema Mwakinyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...