NA JOSEPH MPANGALA, RUANGWA/LINDI

Kocha wa Timu ya namungo FC,  Bakari Malima (Jembe Ulaya) kutoka wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi  amejigamba kuondoka na Ushindi dhidi ya Timu ya Yanga FC ya Jijini Dar es salaam katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Timu ya Namungo ambayo inaongoza katika msimamo wa ligi daraja la kwanza  inatarajia kucheza na Yanga siku ya jumapili wiki hii wakiwa katika mwendelezo wa kusaka tiketi ya kwenda robo fainali.

Bakari malima anasema anaifahamu Timu ya Yanga vizuri hivyo anauhakika wa kupata ushindi akiwa katika kiwanja cha nyumbani.

“Mimi Yanga nawafaham Nje ndani sidhani kama watapata mteremko kama wanaotarajia na uhakikia kwa kuwa gem yenyewe tunachezea hapa nyumbani tunauwezo wa kufanya Vizuri”amesema kocha Malima.
Licha ya kujiandaaa vizuri timu hiyo inamajeruhi wanne wa kikosi cha kwanza ambapo kocha tayari ameanza kuandaa vijana wengine ili kuweza kuziba pengo la wachezaji hao.

"tatizo lililopo kwenye timu yangu sasa hivi kunamajeruhi kama wanne wa kikosi cha kwanza na niwachezaji tunaowategemea lakini tayari kuna vijana tunawanadaa kuchukua nafasi”

Hata hivyo Malima amewaomba mashabiki wa mikoa ya kusini kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya namungo kama moja ya Timu inayowakilisha Mikoa ya Kusini.

Tayari kikosi cha Timu ya Yanga SC kinachojumuisha wachezaji 20 kimeondoka jijini  Dares salaam Ijumaa asubuhi ya kuelekea wilaya ya Ruangwa Mkaoni Lindi tayari kucheza na timu ya Namungo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...