Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akihimiza uzingatiaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa Umma nchini mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa sehemu ya mapokezi kusaini kitabu cha mahudhurio wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanywa na Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo na kuwahi kazini.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uadilifu wa ofisi hiyo wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanyika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo kwa watumishi wa umma nchini.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Constantino L. Kinawiro (mwenye suti) akipongezwa na mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo.

…………………………..

Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo, imefanya ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na kiwango cha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kuhimiza watumishi wa umma nchini kuzingatia waraka huo mahala pa kazi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao unawaelekeza watumishi wa umma aina ya mavazi wanayostahili kuyavaa mahala pa kazi.

Bibi Mishinga amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi ni msimamizi wa miongozo mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambapo kanuni ya kwanza inaelekeza utoaji wa huduma bora na kuongeza kuwa moja ya kigezo cha watumishi wa umma kutoa huduma bora ni pamoja na kuvaa mavazi yenye staha.

Bibi Mishinga amefafanua kuwa, zoezi hilo la ukaguzi katika ofisi ya Rais-Utumishi limebaini kuwa asilimia 95 ya watumishi wameonekana kutekeleza vema waraka huo wa mavazi ikiwemo kuwahi kazini na asilimia tano ya watumishi waliobainika kutotekeleza waraka huo wamekumbushwa kuuzingatia.

Aidha, Bibi Mishinga ametoa wito kwa wasimamizi wa taasisi zote za umma nchini kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa waraka huo na kuwahimiza watumishi walio chini yao kuwahi kazini kwa ili kutoa huduma bora na kwa wakati kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyohimiza.

Bibi Mishinga amesisitiza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ndio msimamizi wa waraka huo wa mavazi itaendelea kufanya ukaguzi na ufuatiliaji katika taasisi zote za umma nchini na haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wa umma watakaobainika kuukiuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...