Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) wakitoa elimu kuhusu uchunguzi wa uvimbe kwenye matiti kabla ya kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na watalaam wa hospitali hiyo. 
Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 
Mtaalam wa Radiolojia Dkt. Ndigwake Mallango akimuelekeza Bw. Diatrick Luoga mkazi wa Kimara namna ya kujifanyia uchuguzi wa awali wa uvimbe kwenye matiti. 
Dkt. Irene Godlove akimsajili Bi. Sadia Sinani kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa awali wa uvimbe kwenye matiti. Huduma hiyo inatolewa bure leo na kesho hospitalini hapo. 


Dar es salaam 

Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. 

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa atagundulika kuwa ana uvimbe, sampuli itachukuliwa kwa njia ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

Hivyo ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa uchunguzi wa awali ambao unafanyika leo na kesho na huduma hiyo inatolewa bure. 

Akielezea kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti Dkt. Sakafu amesema saratani ya matiti ni namba mbili kati ya saratani zinazowapata wanawake hapa nchini, pia katika vifo vyote vitokanavyo na saratani kwa wanawake Saratani ya matiti ni ya pili. 

“Wengi wanafika hospitalini kwa kuchelewa na ugonjwa unakua umefika hatua ya mwisho na hivyo kusababisha matatibabu yake kuwa na changamoto’’. Amesema Dkt. Sakafu. 

Kwa upande wake Daktari kutoka MEWATA, Dkt. Deograsia Mkapa ametaja visababishi vya ugonjwa wa saratani ya matiti kuwa ni kutonyonyesha, kutofanya mazoezi mara kwa mara na uvutaji wa sigara. 

Dkt. Mkapa amewashauri wanawake endapo wakiona mabadiliko yoyote kwenye mwili hasa kwenye matiti kuwahi hospitalini kwa ajili ya uchunguzi. 

Katika zoezi hilo zaidi ya watu 70 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...