*Ni baada ya eneo la awali walilolipata la  kuambiwa kuna shughuli nyingine itafanyika
*Ilikuwa lifanyike viwanja vya Posta Kijitonyama Aprili 21, 2019

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

KAMATI ya Tamasha la Pasaka chini ya Msama Promotion limesema kwa sasa bado linaendelea kutafuta eneo la kufanyia tamasha hilo katika Jiji la Dar es Salaam baada ya eneo la awali kupangiwa shughuli nyingine.

Awali tamasha la Pasaka kwa mwaka huu wa 2019 lilipangwa kufanyika eneo la Viwanja vya Posta Kijitonyoma jijini Dar es Salaam Aprili 21, lakini Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo imepata maelekezo kuwa eneo hilo eti limepangiwa shughuli nyingine, hivyo wameanza kutafuta eneo jingine.

Akizungumza jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Msama Promotion  Alex Msama amewaambia waandishi wa habari baada ya kuambiwa eneo hilo siku ya Aprili 21 kutakuwa na kazi nyingine, kamati imeanza kutafuta eneo jingine hasa kwa kuzingatia tamasha hilo kwa mwaka huu linatakiwa kuanzia katika Jiji hilo.

“Mwaka huu kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka liliamua kuwa tuanze jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Posta, hata hivyo tumeambiwa kuwa siku hiyo kutakuwa na shughuli nyingine.Kamati imeanza kutafuta eneo jingine ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika Dar es Salaam.

“Kuna maeneo mawili ambayo tunaendelea kuyafuatilia kwa ajili ya kufanikisha tamasha la Pasaka kwa Mkoa wa Dar es Salaam.Hata hivyo kwa sasa naomba nisiyataje kwani bado mazungumzo kati ya kamati yetu na wahusika yanaendelea na tutakapofanikiwa tutaeleza ni wapi,”amesema Msama.

Amesisitiza ukweli kwa Dar es Salaam tamasha la Pasaka halijafanyika kwa muda mrefu sana, hivyo walioona mwaka huu lifanyike na ukweli bado hawajakata tamaa kwani wanaamini litafanyika kama ambavyo wamekusudia na pale itakaposhindika basi tamasha hilo litaanzia mkoani na kisha wataangalia namna nyingine ya kulifanyia na Dar.Msama amesema  ni matumaini yake kuwa wenye kutoa kibali cha kutoa maeneo ya kufanyia tamasha hilo watatoa kibali kwani mazungumzo yanaendelea vizuri.

Kuhusu tamasha hilo, Msama amesema malengo yake ni yale yale ya kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani pamoja na kufanya maombi kumuombea Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli ili aendelee kuwa na afya njema na hatimaye kuendelea kuwatumikia Watanzaia.

“Kuna mambo makubwa ambayo Rais wetu ameyafanya ndani ya kipindi kifupi, kuna miradi mikubwa ya maendeleo inaendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa reli ya kisasa ya SGR  na ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji. Kwa kazi anayoifanya Msama Promotion kupitia tamasha la Pasaka tunaona ni wakati sahihi kutumia tamasha hilo kuungana na watanzania wengine kumuombea Rais.

“Pia huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, hivyo Tamasha la Pasaka litajikita katika kuiombea nchi yetu iendelee kuwa na amani na kuvuka salama kwenye uchaguzi huu wa Serikali za mitaa.Tamasha la Pasaka baada ya kuanza jijini Dar es Salaam tutakwenda na mikoa mingine,”amesema Msama.
Kwa upande  wake Mmoja wa Waratibu wa Tamasha la Pasaka Salehe Mohamed amesema tamasha hilo awali ilikuwa lifanyike Kijitonyama, lakini kuna shughuli nyingine itafanyika siku hiyo katika eneo hilo.

    Tunawaomba wananchi wa Dar es Salaam na mikoa mingne ambako tamasha la Pasaka litafanyika wajitokeze kwa wingi, usalama ni wa kutosha na vyombo vya ulinzi vimejipanga , hivyo kuhusu usalama ni wa kiwango cha hali ya juu sana.Tunafahamu nchi yetu kuanzia Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dk.John Magufuli amehakikisha nchi yetu inakuwa salama.Pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekuwa mstari wa mbele kulinda usalama wa raia na mali zao,”amesema.

Amefafanua kuwa Lazaro  kuna mambo mengi ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.Magufuli yamefanyika na kupitia tamasha la Pasaka wanakila sababu ya kuwaambia Watanzania mambo mazuri yaliyofanyika nchini kwetu.

“Tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwani badala ya kusimuliwa mambo mazuri yatakayopatikana kwenye tamasha la Pasaka ni vema wakaja wenyewe ili waone, wasikubali kusimuliwa,”Amesema Mohamed.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam leo ofisini kwakwe Kinondoni kuhusu maandalizi wa tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama akimsikiliza mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Saleh Ali wakati akifafanua zaidi kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 21 jijini Dar es salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...