Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa vyanzo vya maji ni lazima visimamiwe kuhakikisha rasilimali hiyo ya maji inapatikana ya kutosha na inakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Huduma ya upatikanaji wa maji ambayo kupitia watoa huduma hiyo hususani mamlaka za maji, yanatokana na uhifadhi unaofanywa na Bodi za Maji za Mabonde (ambayo ni 9) yaliyopo nchini ambapo yanayotekeleza Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde Wami/Ruvu Hamza Sadiki wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Warsha Maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa Usimamizi na Utunzaji wa Rasilimali za Maji iliyoandaliwa na Bodi.

Amesema Bodi hiyo ndio wasimamizi wa vyanzo vyote vya maji vilivyopo kwenye Bonde la Wami/Ruvu ambalo linapita kwenye mikoa 7 ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Manyara, Tanga na…hivyo ni lazima wasambazaji wote wa maji hayo wapate kibali kutoka bonde hilo.

Akisisitiza kuwa wananchi wengi wana uelewa mdogo kuhusiana na uhifadhi wa maji na kusababisha vyanzo hivyo kuingiliwa na shughuli mbalimbali za kibidamu zikiwemo uvuvi, kilimo pamoja na ufugaji.

“Vyanzo vya maji nchini chanzo kikuu ni mvua, hivyo kila mmoja akivuna maji ya mvua. Mwisho wa siku maji hayo yanayohifadhiwa chini ya ardhi na kutumika kama vyanzo vya chini na juu ya ardhi yatakosekana”, amesema Mwenyekiti.
Mwakilishi wa Afisa wa Maji wa Bonde la Wami\Ruvu Mshuda Wilson amesema kuwa visima vinavyochimbwa vinatakiwa kuwa na kibali kuendelea kumiliki kisima hicho ni kosa la kisheria.

Sheria inakataa uchafuzi wa mazingira na inapotokea mtu anachafua maji ikiwemo utiririshaji maji maji katika vyanzo vya maji yatakiwa kuipimwa na ndipo yaweze kurudishwa katika vyanzo hivyo. Amesema shughuli za kibidamu katika ndani ya mita 60 ya vyanzo ya maji zinazuiliwa kufanyika na kuwepo shughuli hizo ni kinyume cha sheria ya maji ya usimamizi wa rasilimali za maji. 

Amesema kuwa maji ya mvua nayo uvunaji wake unaangaliwa kwa kiwango endapo kiwango kitazidi zaidi lita 20,000 lazima uvunaji wa maji hayo yapate kibali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Hamza Sadiki. Akizungumza na waandishi wa Habari wa akifungua warsha ya Bonde la Wami/Ruvu

 Mwakilishi wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Mshuda Wilson akitoa taarifa Bonde la wami/Ruvu katika warsha ya waandishi habari kuhusiana na uhifadhi wa vyanzo vya maji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...