*Asema
ushindi wa Taifa Stars ni wa Watanzania wote
*Asisitiza sasa timu yoyote itakayokuja nchini itapigwa tu
Na
Said Mwishehe,Globu ya jamii
KAMATI
ya Saidia Taifa Stars ishinde yenye wajumbe 14 wakiongozwa na Mwenyekiti wao Paul
Makonda imetoa shukrani kwa Watanzania wote kwa kufanikisha timu ya Taifa ya
Tanzania 'Taifa Stars' kushinda mechi yake dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda.
Taifa
Stars waliifunga Uganda mabao 3-0 na hivyo kufanikiwa kuipeleka Tanzania nchini
Misri kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019.Ushidni wa Taifa Stars umeifanya nchi
yetu kuandika historia ya aina yake baada ya miaka 39.
Akizungumza
leo Machi 26,2019 jijini Dar es Salaam Makonda amesema Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde inatoa
shukrani kwa makundi mbalimbali kwa kufanikisha ushindi huo ambao ni Watanzania
wote.
"Nitoe
shukrani kwa wapenzi ,wakereketwa na
wadau wote wa michezo. Walihakikisha Taifa Stars inashinda kwa kushiriki kwenye
dua na sala.Kamati yetu ilikuwa na kazi kubwa mbili , kwanza ni kuhakikisha
Taifa Stars inashinda na mbili kufuatilia mchezo mwingine wa Lethoto na Cape
Verde.
"Baada
ya Rais wa TFF kuteua kamati hii tulihakikisha hatukuangushi na tunafahamu tulipoteza mechi
yetu dhidi ya Lethoto ambako kwa sehemu fulani kulikatisha tamaa.Tuliwepa kazi
ngumu,"amesema Makonda.
Amefafanua
ili kuhakikisha kamati inatimiza majukumu yake ilichukua jukumu la kuunda
makundi mbalimbali yakiwamo ya watu mashuhuri, mastaa katika tasnia ya sanaa
nchini, wanamichezo wa zamani, wenye mahoteli, wenye baa,vyombo vya habari na
wenye vyombo vya usafiri.
Amefafanua
katika nchi yetu klabu za Simba na Yanga ndivyo vyenye mashabiki wengi wa soka,
hivyo aliona haja ya kuwachukua Haji Manara na Jerry Muro ambao nao aliwaita
kwenye kamati hiyo na hakika wametoa mchango mkubwa katika kusaidia kuunganisha
mashabiki wa vilabu hivyo.
Makonda
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema pamoja na kazi hiyo Kamati
yao ilihakikisha inairudisha timu ya Taifa Stars kwa Watanzania na kazi hiyo
imefanikiwa kwani hapo awali ilionekana kama vile haina mwenyewe na baada ya
hapo ndipo likaja wazo la kutafuta watu mashuhuri.
"Kazi
ya pili ilikuwa kuzungumza na vyombo vya habari kusaidia kuhamasisha. Jambo la
tatu ni kuhamasisha kwenye maeneo yenye watu wengi kama baa, hoteli na vyombo
vya usafiri ili nao wato ruhusa ya kujadili kwa mchezo wa Uganda na Tanzania
kama sehemu ya kuhamasisha.Kazi ambayo imefanikiwa na wote
tumeona,"amesema Makonda.
Amefafanua
ushiriki wa makundi hayo ya kufanya kazi ya kuhamasisha, Uwanja wa Taifa
ulizidiwa kwa idadi ya watu ambapo ametumia nafasi hiyo kuomba radhi kwa wote
waliokuwa na tiketi zao lakini hawakuingia uwanjani na kwamba wamejifunza ,
hivyo watajipanga isitokee tena.
"Kwa
namna ambavyo walijitokeza kwa wingi uwanjani maana yake Watanzania wanapenda
mpira na michezo mingine yote. Tutaendelea kushauri ikiwemo ya tiketi kukatwa mapema
na pale ambapo uwanja utakuwa umejaa basi watu wambiwe mapema,"amesema
Makonda.
Pia
amempongeza Kocha wa Taifa Stars kwa kupanga kikosi kizuri cha ushindi na
kufafanua zawadi ya viwanja ambayo imetolewa na Rais Dk.John Magufuli wataweka
uratatibu utakaosaidia hata wale wachezaji ambao walikuwemo kwenye ile michezo
ya awali nao wanapewa.
"Kwa
namna ambavyo Watanzania wamehamasisha na timu yetu ya Taifa, nina uhakika timu
yoyote itakayokuja Uwanja wa Mkapa lazima itapigwa tu.Mashabiki ni mchezaji wa
12 na sasa tunao , hatuna wasiwasi na timu yetu,"amesema Makonda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...