Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda @baba_keagan amemkabidhi Kijana Ikuzi Kicheko muhamasishani Mzalendo Kitita cha Shilingi Milioni 1 Baada ya Kujitolea Kutembea Kwa Mguu Kutoka MANYARA Mpaka DAR Kuja Kuhamasisha Ushindi Kwa Taifa Stars,Lakini Pia Viongozi wa TFF Wameahidi Kumpatia Zawadi zaidi na Kwa Kuanzia Wamempa Nguo Zikiwemo Jezi Original za Taifa Stars na Mpira Ili akirudi Mkoani Manyara Watu Wasimshangae na Kumkataa Tena Njiani.
 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMATI ya Saidia Taifa Stars ishinde imesema baada ya kufanikisha ushindi wa Taifa Stars sasa inaelekeza nguvu zake kuweke mikakati ya ushindi kwa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys inayojiandaa kushiriki kushiriki mashindano ya AFCON Under 17.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuna mashindano makubwa yanakuja ya AFCON Under 17 ambayo yatafanyika nchini Tanzania.

"Tunawaomba Watanzania tuendelee kushikamana na kuonesha umoja wetu kwa kuhakikisha timu yetu ya vijana inashinda michuano ya AFCON na kupata tiketi ya kwenda kushiriki kombe la Dunia la vijana linalotarajia kufanyika nchini Brazil.

"Tuna uhakika kwa umoja wetu na kwa mapenzi ya Mungu tutakwenda Brazil.Kikubwa ni kuwapa hamasa wachezaji wetu wa Seregeti Boys watafanya vema, katika mashindano ya AFCOM under 17 tunahitaji kushinda mechi mbili tu , tuna uhakika tutashinda na Kamati yetu imejipanga na tutaendelea kupeana taarifa kila kinachoendelea,"amesema Makonda.

Pia amesema kuwa Aprili 5, mwaka huu timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' nayo inacheza na ni jukumu la Watanzania kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwa kuinga mkono. "Tuna uhakika Taifa Stars itashinda katika mchezo wa Aprili 5, 2019 kwani katika Uwanja wa Mkapa yoyote atakayekuja atapigwa tu,'amesema Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...