Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BAADHI ya watu wana matatizo au hali za chini katika kuelewa lugha hasa katika maandishi na kuongea, wataalamu wengi wamefanya tafiti nyingi ya kutambua matatizo hayo likiwemo la Disigrafia.

Imeelezwa kuwa disgrafia ni tatizo linalompata mtu ambapo hushindwa kuandika na kuelewa maandishi na michoro, mtu mwenye tatizo  hili hushindwa kuumba herufi na anakuwa na mwandiko mbaya.  Aidha mtu mwenye disigrafia hushindwa kuwasilisha mantiki katika karatasi.

Watu wengi huwa na matatizo katika kuandika ila disigrafia ni zaidi ya hapo kwani tatizo hilo hugusa mifumo ya fahamu na hujitokeza wakati mtoto anapoanza kujifunza kuandika, mfano: katika daftari lenye mistari anaweza kuandika sentensi moja katika mistari minne huku akichanganya herufi kubwa na ndogo na zenye ukubwa tofauti tofauti.

Tatizo hili humfanya mtu kushindwa kubadili sauti za lugha kuwa herufi za maandishi, kushindwa kutambua herufi au kuandika kinyume mfano: d kuwa b au z kuwa 3.

Dalili za mtu mwenye tatizo hili ni pamoja na; kugeuza herufi, maandishi yasiyolingana ukubwa, kuchanganya herufi na namba na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.

Pia mwenye tatizo hili anaweza kuandika maneno yasiyokamili mfano; Mama anapk,  kushika vibaya viandikio kama kalamu na peni. Aidha mtu mwenye tatizo hili huandika mwili ukiwa unacheza, kuzungumza kila anachoandika na kupata ugumu wa kuunganisha mawazo.

Na inasemekana kuwa watu wenye tatizo hili huzungumza vizuri kuliko kuandika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...