Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akikabidhi kikombe kwa Mshindi wa kuvuta kamba kitengo cha Mita Tanesco katika bonanza la michezo liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya General Tyre ,kulia ni Nahodha wa timu hiyo Innocent Pascal.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa pete ya RAS ,Grace Kija akipokea zawadi wa kombe kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro.
Nahodha wa Timu ya mpira ya Ras akipokea zawadi ya kikombe ,baada ya kuifunga timu ya Tanesco goli 2 kwa 1.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya RAS wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa pete baada ya kukabidhiwa zawadiWachezaji wakisakata kabumbu kati ya Timu ya TANESCO na timu ya RAS
Mashindano ya kuvuta kamba kati ya Timu ya Tanesco na RAS ambapo TANESCO iliibuka na ushindi katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha
Michezo ikiendelea hapa timu zote wakivuta kamba katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha


Na Vero Ignatus, Arusha.


Shirika la Umeme Tanesco mkoani Arusha limefanya bonanza kubwa la michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na kukimbiza kuku huku wadau wengi wakijitokeza kwenye viwanja vya General tyre kushughudia michezo hiyo.

Akifungua Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema kuwa michezo ni afya ,ajira na furaha katika jamii hivyo bonanza hilo la Tanesco linalenga kuhamasisha wananchi kuunga mkono timu ya Vijana ya Taifa ya Serengeti ambayo inashiriki katika michuano ya Afcon.

Daqqaro amesisitiza kuwa michezo inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza kama presha,kisukari na saratani ambayo husababishwa na aina ya maisha isiyozingatia mazoezi na lishe.

Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha Donasiano Shamba amesema kuwa bonanza hilo linahusisha michuano mikali kati ya timu ya Tanesco na RAS arusha ambao walichuana katika mpira wa miguu na mpira wa pete.

Shamba amesema kuwa michezo hilo inalenga na kujenga na kudumisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali ili kuleta maendeleo na pia kuunga mkono juhudi za Timu zinazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa ikiwemo Serengeti.

Mmoja kati ya washiriki wa Bonanza hilo Innocent Pascal ameshauri waandaaji kuandaa michezo hiyo mara kwa mara ili kuibua vipaji vya michezo ambavyo vinaweza kuleta medani za heshima za kitaifa na kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...