Bi. Neema Mtemvu, Afisa Uhusiano (TBS), akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibaoni wakati TBS ilipotembela shuleni hapo kutoa elimu juu bidhaa hafifu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwashungu, wakisikiliza elimu juu ya masuala yahusuyo viwango vya ubora, kutoka kwa maafisa Wa TBS.
Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti ubora Mwandamizi (TBS), akizungumza na wajasiriamali wilayani kilombero kuhusiana na utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
Bi Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) akizungumza na wananchi wa soko kuu la Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS.

……………………………..

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetembelea shule ya sekondari Kibaoni pamoja na Shule ya sekondari ya Kwashungu wakati wa Kampeni yake ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizo na ubora katika Wilaya ya Kilombero. 

Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu, amefafanua umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa wajasiriamali wadogo.

Bi Gradness amesisitiza kuwa jukumu la kupiga vita bidhaa hafifu katika Taifa ni la kila mtu, hivyo aliwaasa wawe mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi.

Kwa upande wake, Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaoni, Bw. Kalinga aliwapongeza TBS kwa kufika shuleni hapo kwani ni mkakati mzuri ukizingatia shule huwa na wanafunzi wengi na wanaoishi maeneo mbalimbali hivyo ikiwa kila mmoja atasambaza ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki utakuwa umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Mwalimu Kalinga pia hakuacha kutoa wito kwa TBS kuendelea na zoezi hilo kwani linajenga msingi mzuri kwa vizazi vijavyo na kutengeneza jamii yenye tamaduni ya kujali ubora.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika Soko kuu la Ifakara lenye viunga 515 na maduka 105, pamoja na maeneo ya madukani Ifakara mjini, huku jumla ya wanafunzi 2,089 na walimu 78 wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora .


Sambamba na hayo, TBS ilitoa semina kwa wajasiriamali wapatao 23 katika ukumbi wa halmashauri ya mji Ifakara, ambapo Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza wajasiriamali kufuata utaratibu waliolekezwa ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure bila gharama yoyote, kwani ni fursa ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji kuweza kushindana na kuuza ndani na nje ya nchi . Vilevile wasisite kutuma maombi TBS kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yatolewayo kwa wajasiriamali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hongera sana TBS kwa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa zilizo bora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...