Kaimu Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jesca Shengena akitoa maelekezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Mungu Mfalme, Makange Kitua (kushoto), wakati wa zoezi la Uhakiki wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini linaloendelea katika Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa wa Kitengo cha Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Ngalawa akihakiki taarifa za Taasisi ya Kidini ya Peaceful Life Ministries wakati wa zoezi hilo linaloendelea Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Paskazia Makofi.
Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Mungu Mfalme, Makange Kitua akitoa maelezo ya taasisi yake kwa Afisa wa Kitengo cha Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Ngalawa (kulia), wakati wa zoezi la uhakiki linalofanyika Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kitengo cha Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Thomas Sanira akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Istiqama, Issa Suleiman(kulia), wakati wa zoezi la uhakiki wa taasisi hizo linaloendelea Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Imekuwa ni mchezo wa watu wengi hasa wanaojiita wakristo kuanzisha makanisa ya uongo na kweli kwa manufaa yao. Unakuta wanawatumia vibaya watu masikini na wao wanatajirika mpaka wananunua ndege. Serikali ingekontro utitiri wa makanisa yanayoanziskwa bila mipangilio badala ya kuanza kuhakiki.
ReplyDelete