Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MGAHAWA wa pili wa ukubwa duniani KFC "Kentucky Fried Chicken" umepata umaarufu duniani zaidi kwa bidhaa zake zinazopendwa na wengi zikiwemo kuku wa kukaanga ambao ndio wamebeba jina la mgahawa huo pamoja na bidhaa nyingine kama vile; vibanzi, kifungua kinywa, vinywaji pamoja na maziwa.

Ukiwa na makao makuu huko Lovisville umekuwa  mgahawa wa pili kwa ukubwa duniani  kwa kipimo cha mauzo baada ya McDonald's ambapo KFC imeenea katika maeneo zaidi ya 22,621 duniani na nchi zaidi ya 136 kwa tafiti za mwaka 2018 na una huduma maarufu za Pizza Hut, Taco Bell na Wing Street.

Historia ya mwanzilishi wa KFC inawasisimua wengi kutokana na mapito yake kuelekea mafanikio yake,  Colonel Harland Sanders alizaliwa mwaka 1890 akiwa anaishi na baba yake na alipotimiza miaka 6 tuu baba yake alifariki dunia na kumwachia majukumu ya kupika na kulea ndugu zake, akiwa Sekondari aliacha shule na kurudi nyumbani na kujihusisha na shughuli za kilimo.

Akiwa na miaka 16 Sanders  alidanganya umri ili aweze kujiunga na jeshi na aliachishwa baada ya kugundulika mwaka moja baadaye.

Baada ya kuachana na shughuli za jeshi alipata kibarua katika shirika la reli na alifukuzwa baada ya kugombana na mfanyakazi mwenzake, Licha ya kubahatika kusoma sheria  akiwa kibarua katika shirika la reli  alipoteza sifa ya fani hiyo baada ya kugombana tena hali iliyomlazimu arudi kwa mama yake ambapo alipata kazi katika kampuni ya bima ambapo alifukuzwa kazi hiyo kwa udanganyifu ila hakukata tamaa.

Mwaka 1920 alianzisha kampuni ya usafirishaji wa majini lakini haikidumu, akiwa na miaka 40 alianza kuuza kuku katika vituo, hoteli, barabarani na migahawa ya jirani, na alipoanza kutangaza biashara hiyo alipata upinzani mkubwa miaka 4 baadaye alinunua hoteli ambayo vita vya pili vya dunia vilipelekea kufungwa kwa hoteli hiyo.

Baada ya vita alianza kutangaza biashara yake na ilikataliwa mara 1,009 na hapo ilikiwa tayari na chapa ya KFC na huduma zikiwa zimeboreshwa kwa hali ya juu.

Baada ya kushindwa kote huko Sanders alifanikiwa kushika soko la dunia akiwa anapata mapato ya dola milioni 23 kwa mwaka 2013.

Akiwa na Miaka 90 Sanders alifariki dunia kwa ugonjwa wa Pumu akiacha KFC ikiwa imeenea katika maeneo 6000 duniani na nchi 48.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...