Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam comred Mama Ketty Silvia Kamba leo hii tarehe 26.05.2019 wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2018/2019 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala Muheshimiwa Mussa Azzan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Segerea Muheshimiwa Bonnah Kamoli

Mwenyekiti wa Mkoa aliongozana na Ndugu Yusuph Nassor (MNEC MKOA), Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Zakaria Mwansasu, Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Simon Mwakifwamba  na Ndugu Iddi Azzan

Katika taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika majimbo haya wawili mambo mengi yamefanyika katika miradi mbalimbali (Afya,Elimu,Miundombinu,Maji) ambapo asilimia kubwa ya miradi mmetekeleza na kumalizaka kwa kiwango kukubwa sana.

Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam inampongeza kwa dhati Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Muheshimiwa DKT John Pombe Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani katika ngazi ya Taifa lakini pia kuhakikisha pesa za maendeleo   zinakuja katika majimbo na halmshauri nchini kote.

Pili, kamati ya siasa ya mkoa inawapongeza wabunge wote wa wawili kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini pia kuhakikisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2018/2019 inasomwa na kuwasilishwa.

Mwisho, kamati ya siasa inaipongeza kamati ya siasa ya wilaya ya Ilala ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM wilaya Ndugu Ubaya Chuma kwa kufatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya wilaya ya Ilala

Viva Muheshimiwa John Pombe Magufuli

TUMEAHIDI,TUMETEKEZA

Imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam

26.05.2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...