NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO
SHIRIKA linalosaidia watu wenye maisha duni na kuleta mabadiliko
chanya katika jamii (WHO IS HUSSAIN?), tawi la Dar es salaam kwa
kushirikiana na diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani ,limetoa
msaada wa vyakula kwa kaya 200 zilizopo kwenye kata hiyo,uliogharimu
sh.milioni kumi.
Kila kaya kati ya hizo imepatiwa box lenye vitu vilivyogharimu sh.
50,000 ,ikiwemo mchele kilo 3, maharage kilo tatu, sukari kilo 3,
majani ya chai, tende na tambi ili kuwasaidia katika mwezi mtukufu wa
Ramadan.
Akikabidhi msaada huo, mratibu msaidizi wa shirika la Who is Hussain?,
tawi la Dar es salaam Meesam Bandali amesema,walengwa ni watu wasio na
uwezo wakiwemo wenye ulemavu,wazee katika kaya 200 kata ya Vigwaza.
Awali diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani, amelishukuru shirika
hilo kwa kumfuata kumuomba kupeleka msaada kwa kaya zinazoishi kwenye
mazingira magumu.
Nae msemaji mkuu wa who is Hussain? Iffet Thawer ameeleza Hussain ni
mjukuu wa mtume Mohammad S.W.A. ambae alipinga dhuluma hivyo kuwa
chanzo cha wao kuhamasika kufanya shughuli za kusaidia jamii ikiwa
sasa ni miaka kumi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...