Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amezungumza na wakuu wa mikoa minne nchini na kuwauliza maswali ya papo kwa papo akiwa Makao Makuu Shirika la Simu Tanzania(TTCL) jijini Dar es Salaam kwa kutumia mfumo wa  "Video Conference".

Wakuu wa mikoa ambao Rais Magufuli amezungumza nao kwa mfumo huo ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Rais Magufuli amezungumza nao leo Mei 21,2019 ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mfumo wa mawasiliano wa 'Video Conference' ambao umeunganishwa kwa wakuu wa mikoa yote nchini  ili kuweza kufanya kikao na Rais.

Akizungumza wakati anazungumza na wakuu hao wa mikoa pamoja na mambo mengine aliuliza kuhusu hali ya mvua na upatikanaji wa mazao kwa msimu huu wa kilimo ambapo wakuu hao wa mikoa wamemhakikisha Rais pamoja na uhaba wa mvua lakini wakulima wameanza kuvuna mazao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe,amemwambia Rais Magufuli kuwa Mkoa huo mazao yamepatikana ya kutosha licha ya kuwepo kwa uhaba wa mvua lakini Mkoa wao walipata mvua za kutosha.

Rais Magufuli alimuuliza ni mazao gani yamepatikana kwa wingi ambapo alijibu ni mahindi,mpunga,maharagwe na mazao mengine ya chakula na biashara.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alimwambia Rais kwa Mwanza iko salama na kwamba leo wanaadhamisha miaka 23 tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba iliyozama katika Ziwa Victoria," amesisitiza.

 Rais alimuuliza kuhusu ujenzi wa meli ya kisasa iwapo mkandarasi ameanza kazi ambapo Mongella amejibu mkandarasi tayari ameanza kazi.

"Mheshimiwa Rais mkandarasi ameanza kazi na ana mwezi mmoja sasa.Kazi inakwenda vizuri sana

Hata hivyo Rais Magufuli alitaka kufahamu kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya Ukara wilayani Ukerewe,Mongella amejibu ujenzi umefika hatua nzuri kwani wanatarajia kuanza kuwekamilango na madirisha.

Rais Magufuli pia alitaka kujua hali ikoje kwa TTCL Mkoa wa Mwanza ,amejibiwa kuwa shirika hilo linakwenda vizuri na idadi ya wateja ni kubwa na hivyo kuweza kuchangia pato la Taiga.

Wakati huo huo Rais Magufuli amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ambapo Rais aliuliza kuhusu mvua ambapo alijibiwa kwamba Mkoa huo kuna ukame na hivyo hali ya kilimo sio nzuri sana.

 Hata hivyo Rais alimuuliza Mwanri iwapo ataomba chakula ,amejibu hawezi kuomba chakula kwani wamejipanga na ukame.ambapo ameuzungumzia sio mkubwa sana na kufafanua wanaendelea kuhamasisha wananchi kutunza chakula na kulima mazao yanayostahimili ukame.

"Kuomba chakula siwezi kuruhusu hilo.Kwa sasa tunaendelea kuhifadhi chakula kutokana na ukame.Tunawahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame," amesema Mwanri.

Wakati huo huo Rais alitaka kujua kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Nzega hadi Tabora ,ambapo Mwanri amesema ujenzi unakwenda vizuri.

Baada ya kuzungumza na wakuu hao wa mikoa minne,Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakuu wa mikoa yote nchini kuitangaza TTCL kwani ni shirika la Watanzania.

"Niwaombee Watanzania tuendelee kulitumia shirika la TTCL,ni shirika letu na lazima wote tuliunge mkono kwani kwa kufanya hivyo ni kumue zi kwa vitendo Baba wa Taiga Mwalim Julisu Nyerere kwa kua zisha shirika hilo," amesema Rais Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...