MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imebatilisha  kifungu cha sheria cha  7(3)kinachowaruhusu Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamizi wa Uchaguzi nchini. 

 Uamuzi huo umetolewa Mei, 2019 na Jaji Atuganile Ngwala kunatokana na kesi namba 8 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na   Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Bob Chacha Wangwe.

Aidha katika maamuzi hayo Jaji Ngwala,  ametengua kifungu cha 7 (1) kinachoruhusu mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi na kusema kuwa sheria hizo ni batili na kinyume cha katiba ya nchi.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Ngwala amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo na mpeleka maombi kuwa wasimamizi wa chaguzi ni wanachama wa chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanamaslahi kwenye chaguzi hizo.

Mpeleka maombi (Bob) katika kesi hiyo amewakilishwa na Wakili Fatma Karume, ambae aliwasilisha ushahidi wa majina74 ya wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa (CCM). Kama ushahidi wa dhidi ya shauri hilo.

Jaji Ngwala amesema kuwa sheria  hizo hazijaelekeza utaratibu wowote wa kuhakiki kuwa wasimimizi hawana maslahi binafsi na uchaguzi.

Amesema ya Kuwa  sheria hii ya Tume ya Uchaguzi imekataza mtu yoyote ambaye ni mwanachama wa chama chochote kuwa  haruhusiwi kuwa msimamizi wa Uchaguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...