Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MASHABIKI na wapenzi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi na kuujaza uwanja katika mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Sevilla FC inayoshiriki Ligi ya Laliga ya nchini Hispania.

Tayari timu hiyo imewasili nchini usiku wa jana ikiwa na wachezaji 18 na wanatarajia kukipiga na Simba kesho Alhamis ya Mei 23,2019 saa moja jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mmiliki wa Klabu ya Simba Mohamed Dewj 'MO' amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi ili kuujaza uwanja huo kwani kucheza na timu ya Sevilla FC ni heshima kubwa kwao ambayo wamepewa na Sportpesa.

"Klabu ya Sevilla ni kubwa na inafanya vizuri katika Laliga. Mashabiki wa Simba njooni tuujaze uwanja kama tulivyokuwa tukiujaza kwenye mechi za Klabu Bingwa Afrika.Huenda bahati ikawa kwetu tukaifunga Sevilla na tukaandika historia katika madani ya soka la Tanzania.

"Tunafahamu ujio wa Sevilla nchini umegharimu fedha nyingi lakini Sportpesa wameamua kutumia fedha hizo kwa ajili ya kuhakikisha Simba tunacheza na timu hiyo.Ni lazima tuoneshe heshima tuliyopewa na Sportpesa kwa kuujaza uwanja hapo kesho,"amesema MO.

Amesema kujitokeza kwa wingi uwanjani pia itakuwa sehemu ya kuonesha ishara ya furaha ambayo Wana Simba wanayo kwa msimu huu ambao kwao umekuwa mzuri kutokana na timu yao kufanya vema katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kutwaa ubingwa lakini pia katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...