Serikali imepanga kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Ikozi ikiwa ni miongoni mwa Miradi ya Maji 6 inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji awamu ya Pili (WSDP II) katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa yenye lengo la kutatua kero ya upatikanjai wa maji kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Ikonzi mara baada ya kutembelea baadhi ya miradi ya Wilaya ya Sumbawanga, Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amesema Serikali imejipanga kutekeleza na kusimamia mradi huo kwa ufanisi na kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa mfano kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama kwa wananchi walio karibu na mradi huo.
Profesa Mbarawa amesema miradi mingi ya mabwawa nchini imekuwa ikitekelezwa chini ya viwango na ikishindwa kutimiza lengo halisi, akisisitiza wizara itasimamia kwa ukaribu utaratibu mzima na maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo ili liweze kuwa mfano wa kuigwa nchini.
‘‘Mradi huu ulianza Novemba, 2018 chini ya mkandarasi wa Kampuni ya Emirate Builders Ltd kwa gharama ya Shilingi bilioni 2,943,086,780 na ameshalipwa asilimia 15 ya malipo ya awali Shilingi 441,463,017 unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2019’’, Profesa Mbarawa ameeleza.
‘‘Mkataba wa mradi huu unahusisha ujenzi wa bwawa la ujazo wa lita 436,015,120 pamoja na kazi nyingine na awamu ya kwanza unatarajia kuhudumia Vijiji (3) vya Ikozi, Kazwila na Chituo vyenye jumla ya wakazi 14,395 na baada ya hapo huduma itasogezwa mpaka  Kijiji cha Tentula chenye idadi ya wakazi 2,452’’, Profesa Mbarawa amesema.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Sumbawanga, Patrick Ndimbo amesema usimamizi wa kazi ni mzuri, mkandarasi amekuwa akitumia muda mwingi akiwa site na kazi hiyo inaendelea vizuri akitegemea kukabidhiwa kazi hiyo ifikapo mwezi Julai kama mkataba unavyoonyesha.
Awali, Profesa Mbarawa  alitembelea Mradi wa Maji wa mji mdogo wa Laela na kutoridhishwa na mkandarasi anayetekeleza awamu ya pili ya mradi huo na kuagiza aonane na mkandarasi huyo amuone, ili wapange pamoja upya mpango kazi wa utekelezaji wa mradi huo uliotegemewa kukamilika baada ya miezi minne jambo ambalo waziri huyo amelikataa.
Akiwa katika mradi huo ameagiza chanzo kipya cha mserereko (gravity) cha Kimenyanze kitumike baadala ya chanzo cha awali, kwa kuwa nguvu ya umeme wa nishati ya jua (solar) zilizokuwa zimefungwa kushindwa kusukuma maji kutoka kwenye chanzo hicho cha awali kwenda kwenye tenki na kuyasambaza kwa wananchi.
Profesa Mbarawa amesema jumla ya gharama za mradi huo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.7 na zaidi Shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 80 zimeshalipwa, akatoa miezi miwili tu mradi huo uwe umekamilika.
 Sehemu ya mradi
 Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiomngea na wataalamu huko Ikonzi akiwa katika kutembelea baadhi ya miradi ya maji Wilaya ya Sumbawanga.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiomngea na wataalamu huko Ikonzi akiwa katika kutembelea baadhi ya miradi ya maji Wilaya ya Sumbawanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...