Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angella Kairuki amesema kwamba Serikali itatumia watalii wanaokuja kutembelea vivutio vyetu kutangaza fursa zilizopo za uwekezaji katika sekta ya utalii ,biashara na madini.

Angella ameyasema hayo jana  wakati akizungumza na wawekezaji kutoka nchini China katika Kituo cha Mikutano cha AICC kilichopo ndani ya Jiji la Arusha ambapo amesema lengo la mkutano huo nikubadilishana mawazo na uzoefu katika eneo la uwekezaji na kutangaza fursa za kibiashara.
 
Amebainisha kuwa Serikali ya Dk.John Magufuli ipo bega kwa bega na Serikali ya China kujenga jamii yenye ushirikiano na maendeleo.

Amesema kuwa wanakaribisha China kufungua milango kwa Tanzania katika kuwekeza katika mpango mmoja ili kulifikia soko lake kubwa katika sekta zote muhimu kuanzia katika uwekezaji upande wa utalii, biashara, madini na fedha.

"Napenda kuwahakikishia marafik wa China kuwa Tanzania ni ya amani unapokuja kuwekeza Tanzania uwe nauhakika wa usalama wako binafsi, pia tupo tayari kukaribisha uwekezaji kutoka china na kuwahakikishia usalama wa mitaji yenu Kwani tunazosera nzuri na sheria thabiti. "alisema Kairuki.

Amebainisha kuwa Tanzania ni mshirika anaetegemeka na mdau anayeaminika kwa China, hivyo ndio sababu haikua ajali kwa nchi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza za Afrika kuhusishwa katika mpango wa ukanda mmoja wa kibiashara (one belt One road initiative) kwa sababu hiyo hiyo nchi yetu ni miongoni mwa nchi nne vinara chini ya mpango wa uzalishaji na uwezeshaji wa pamoja wa china.

Amewataka watanzania kuitangaza vizuri nchi hususani ni kipindi hichi watalii wanakuja kutembelea vivutio vyetu huku akiwawahamasisha  waandishi wa habari kuona umuhimu wa kuitangaza nchi yao kama vile waandishi kutoka nchini China wanavyofanya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Uratibu,Bunge, Kazi,Ajira na Watu wenye ulemavu Anthony Mavunde amesema Serikali inapenda wageni na wafanyakazi kutoka nje ya nchi kwa kuwa wanasaidia kuongeza ujuzi ila wawapo nchini wanaitajika kufuata sheria

Wakati huo huo KwaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffey Mwambe amesema kongamano hilo litasaidia ukuaji wa uchumi na wao wamejipanga kikamilifu kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini ambazo sasa zimefunguka kwa wingi.

Jumla ya wawekezaji 50 kutoka katika kampuni 25 wameshiriki kongamano hilo ambapo pia wageni hao kutoka taifa la watu wa China 336 watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu  uwekezaji Angela Kairuki katikati akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati akiwakaribisha Wawekezaji kutoka nchin China.
 Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Uratibu,Bunge, Kazi,Ajira na Watu wenye ulemavu Anthony Mavunde akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffrey  Mwambe akieleza jambo mbele ya Wawekezaji (hawapo pichani) kutoka nchini China wakati wa mkutano wao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...