SERIKALI imesema itatoa ushirikiano wa kila aina kwa timu ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo Worries) katika mashindano yatakayoshirikisha nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yameswa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu, Stella Ikupa wakati akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika Ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ikupa alisema Serikali itashirikisha wadau wote pamoja na wabunge ili kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanakuwepo kwa timu hiyo.Alisema wabunge wameanza kwa kukubali kuchangia Shilingi 100,000 sawa na shilingi milioni 40 huku wakiendelea kushirikisha wadau wengine.

"Ninawahakikishia serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mnachukua kombe hilo naomba msituangushe," alisema.Alisema awali walikuwa hawaamini kuwa kuna uwezekano wa watu wenye ulemavu kucheza mpira wa kiwango hicho ila amejionea mwenyewe na kwamba atawapa ushirikiano.

Ikupa alisema katika kuonesha Serikali imedhamiria kukuza michezo ofisi ya Waziri Mkuu itatoa seti tano za fimbo za kuchezea na baiskeli ya walemavu moja ili ziweze kusaidia katika mashindano.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu nchini (TAFF), Rizik Lulida alisema anaishukuru serikali na Spika wa Bunge kukubali kila mbunge kuchangia mashindano hayo.

Lulida ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF) alisema pia TAFF inawaomba wadau mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro kufadhili mashindano hayo."Tumetumia nembo tembo kama jina la timu tukiamini tutawalinda, kuwatangaza wanyama wetu na kuhifadhi vivutio vyetu," alisema Lulida.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo kwa Watu Wenye Afrika Mashariki kwa Waawake na Watoto (CECAAF), Nuru Awadhi alisema mashindano hayo ni muhimu katika kutangaza nchi kimataifa.Awadhi alisema Tembo Worries, watafanya vizuri katika mashindano hayo na kuipongeza serikali kuunga mkono mchezo huo.

Rais wa TAFF, Peter Sarungi, alisema kwa sasa wana program tatu ambazo zipo mbele yao kuhakikisha wanaibuka washindi."Program ya kuingia kambini, mafunzo ya marefa na mkakati wa ushindi hivyo ni imani yangu tukifanikisha haya kila kitu kitaenda sawa," alisema.

Katika wa CECAAF, Moses Mabula alisema alisema shirikisho limejipanga vizuri kusimamia mashindano hayo na kwamba itapendeza kombe likibaki nyumbani.Kwa upande wake Mchezaji Athuman Lubandani alisema wamejiandaa vizuri kuibuka na ushindi katika mash kinda hayo.

"Tunakushuru Mheshimiwa Naibu Waziri na Mama Lulida kwa mchango mnaotupatia hatutawaangusha," alisema
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Stella Ikupa, akizungumza na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Walemavu pichani hawapo, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Riziki Lulida na Kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Walemavu Afrika Mashariki (CECAAF), Nuru Awadhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...