Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara ameziomba Tasisi na Azaki mbalimbali zinazojishughulisha na elimu kuacha na kujifungua na kujitokeza hadharani kutoa maoni juu ya uboreshaji wa elimu nchini.

Waitara amesema hayo akizungumza na wadau wa Maendeleo na Viongozi wa Azaki Mbalimbali katika hafla ya kusherehekea Ushindi wa Haki Elimu katika tuzo ya umahiri wa tasisi za kiaraia Barani Afrika .

Waitara amesema licha ya shirika la Haki Elimu Kuibuka mshindi wa jumla pia ilikuwa mshindi katika vipengele vingine viwilivya umahiri wa kimkakati na unyumbufu yaani Strategic Ability and Adaptability pamoja na uwezo wa uongozi na utawala ,hii inaakisi namna shirika linalojiongoza na kuzingatia misingi iliyowekwa .

"nitoe wito kwa tasisi nyingi za kiraia nchini Tanzania kujifunza kutoka mafanikio ya Haki Elimu ili kufanikisha zaidi kazi zaidi ya kuboresha maisha ya jamii ya watanzania na kuiletea sifa nchi yetu kimataifa hivyo nitafurahi kuona asasi zingine za kiraia zinaibuka vinara kwenye mashindano kama haya" Amesema Waitara.

Alimaliza kwa kusema kuwa uwezo na utayari wa Haki Elimu kufanya kazi na wadau mbalimbali ndio uliowawezesha kupata mafanikio haya na ni imanai yangu kuwa shirika litaendelea kushirikiana na serikali katika harakati za kueleta maendeleo katika sekta ya elimu hapa nchini.
 Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara akizungumza na wadau wa Maendeleo na Viongozi wa Azaki Mbalimbali katika hafla ya kusherehekea Ushindi wa Haki Elimu katika tuzo ya umahiri wa tasisi za kiaraia Barani Afrika .
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Haki Elimu Nchini, Dk. John Kallage akieleza namna tasisi hiyo ilivyoweza kuibuka mshindi katika kategori mbili pamoja na kuepewa ushindi wa jumla wa tuzo hizo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Haki Elimu Nchini, Richard Mabalaakitoa shukrani wa kwa wafanyakazi wa Haki Elimu na wadau wengine kwa kuwapa sapoti.
 Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara,akigonga Chiazi na Baadhi ya Wadau na Wafanyakazi wa Haki Elimu
 Wafanyakazi na Wadau wa Haki Elimu wakifungau Shampeni katika sherehe ya kupongezwa kupata tuzo ya Azaki bora barani Afrika.
Mgeni Rasmi na Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Azaki Mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...