Na Humphrey Shai, Globu ya Jamii, Kigoma.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa Sh bilioni 32.5 kwajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa gati katika bandari ndogo za Ujiji na Kibirizi zilizopo Kigoma mjini.

Pia mradi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la gorofa moja kwaajili ya ofisi za meneja wa bandari za ziwa Tanganyika.

Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya China Railway 15 Group ulianza Februari 28, 2018 na unahusisha ujenzi wa gati la Kibirizi lenye urefu wa mita 250 na kuifanya bandari hiyo kuwa na gati refu kuliko bandari zingine katika Ziwa Tanganyika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ndogo ya Kibirizi, Afisa Bandari hiyo, Ghalib Mahyolo, alisema kwa sasa licha ya kutokuwepo kwa gati la kisasa wanahudumia tani 600,000 hadi 700,000 kwa mwezi.

Pia alisema kwa mwezi mmoja wanahudumia boti zipatazo 220 hadi 260 na boti 70 kati ya hizo ni za abiria ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 50.
Alisema boti za abiria zinahudumia vijiji vitatu ambavyo ni Kagunga, Mwamgongo na Mtanga ambapo usafiri unapatikana siku zote za wiki isipokuwa Jumapili.

Kwa upande wa uwezo wa boti za mizigo zinazohudumiwa bandarini hapo alisema boti kubwa kabisa zina uwezo wa kubeba tani 120 na zinafanya safari katika ya Tanzania, Burundi na DRC."Mradi wa kujenga gati mpya hapa Kibirizi utaongeza biashara ya usafirishaji wa mizigo na abiria kwani itawezesha upakiaji na upakuaji kufanyika kwa urahisi zaidi tofauti na ilivyo sasa," alisema Mahyolo.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, alisema mradi huo ni mkakati wa TPA kuboresha bandari ndogo za maziwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma pamoja na kuongeza mapato.

Msese alisema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa uzio kuzunguka bandari ya Kibirizi ambayo imekuwa na changamoto yakuingiliwa na shughuli zingine za wananchi ambazo si za kibandari ikiwemo kuchota maji katika eneo la bandari.Alisema pia kutakuwa na ujenzi wa jengo la abiria, ghala la kuhifadhia mizigo, vyoo na kibanda cha mlinzi pamoja na uwekaji wa paving.

Akizungumzia mradi huo Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji wa Maboti, Edmond Msabaha, alimshukuru Rais John Magufuli kwa serikali kuptia TPA kuona umuhimu wa kuwajengea gati ku wa la kisasa.Alisema kwa sasa wanapakiza mizigo na abiria kwa shida tofauti na ikiwepo gati la kisasa.

"Mradi hii utakua na manufaa kwetu wasafirishaji na hata wateja wetu lakini pia utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kutokana na kazi kuwa zinafanyika kwa haraka, hivyo nimshukuru Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu," alisema Msabaha.
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Mseseakizungumza juu ya kazi zinazofanywa katika Bandari ya Kigoma na Miradi itakayojengwa katika bandari hiyo
Moja ya Mashine iliyopo katika Bandari ya Kigoma inayonyanyua mizigo kwa haraka ambapo bandari hiyo inaborehsw akwa gharama ya zaidi ya Milioni 30.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...