Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wakazi wa Kawe Mkwamani wanaokaa pembezoni mwa Mto mbezi watakiwa kuacha kuendelea kuchimba mchanga katika mto huo.

Kuchimba kwa mchanga huo kunasababisha madhara kwa wakazi wa eneo kwa kuongeza kingo  na kufanya wakati wa mvua baadhi nyumba kuanguka.

Akizungumza na Wananchi Kawe Ukwamani Afisa wa maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema zuio hilo ni kwa mujibu wa sheria ikiwa ni kulinda mazingira ya Mto  Mbezi na hakuna kibali cha uchimbaji wa mchanga katika Mto huo.

"Nyumba za watu zinabomoka, watu wanachimba wanaenda hadi kwenye kuta za nyumba na kuanguka, hivyo haiwezekani uchimbaji huo ukiendelea katika eneo hili”. Amesema Mhandisi Ngonyani.

Aidha Mhandisi Ngonyani amesema kuwa sheria za rasilimali za maji ya mwaka 2009 namba 11 mwenye mamlaka ya kutoa vibali kwaajili ya watu kuingia mtoni kwaajili ya shughuli yoyote ile ni bonde hasa wao Wami-Ruvu sio halmashauri kwasasa.

Kwa upande wa Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kawe ASP. Dkt. Ezekiel Kyogo amewataka wachimbaji wamchanga wa maeneo hayo  kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili wasiweze kuingia katika matatizo.

 “Kama wanataka kuchimba mchanga wanatakiwa kufuata sheria kwani kila kitu kina utaratibu wake zilizowekwa na kama wakiamua kutofuata sheria basi sheria itachukua mkondo wake”. Amesema ASP. Dkt. Kyogo.
 Baadhi ya nyumba zilizolika kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa katika Mto Mbezi Kawe Mkwamani.
 Mkuu wa Operesheni wa Polisi Wilaya ya Kawe Dkt.Ezekiel Kayogo akizungumza na waandishi habari namna walioyapokea maagizo ya zuio la uchimbaji wa mchanga katika Mto Mbezi,jijini Dar es Salaam.
 Gari lililokutwa katika Mto Mbezi eneo la Kawe Mkwamani likiwa limebeba mchanga ambapo walilikamata Jeshi la Polisi.
 Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akitoa maelezo kwa wananchi Madhara ya uchimbaji mchanga katika Mto Mbezi.
 Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika Mto Mbezi jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...