Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la FORUMCC Rebecca Muna amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha wananchi wote wakiwamo vijana wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia amesema iko haja kwa vijana pamoja na mambo mwngine kutumia fursa ambazo zinazojitokeza kutokana na athari za mabadiliko ya kimazingira na tabianchi kuwa fursa ikiwa pamoja na kujikita katika nishati mbadala .

Muna ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam ambapo FORUMCC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini wameadhimisha Wiki ya Mazingira kwa kuandaa maonesho ya nishati mbadala pamoja na mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu ya kutoka Abby Enviroment & Agriculture Company Service wameibuka washindi wa Kombe la Mazingira,hivyo wametangazwa kuwa mabalozi wa mazingira.

Akifafanua zaidi Muna amesema FORUMCC kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) wana mradi uliojikita katika mabadiliko ya tabianchi na mazingira,hivyo kupitia ufadhili huo wamekuwa mstari wa mbele kuwashirikisha Watanzania kukabiliana na mabadiliko yatabianchi.

"Leo hii ikiwa tunaadhimisha wiki ya mazingira FORUMCC tumeona tunakilasababu kuwakutanisha vijana ambao ni wadau wa mazingira kwa kuwaandalia michezo wanayoipenda na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa vijana.

" Kupitia siku hii ya leo ya kuadhimisha wiki ya mazingira tunawapa ujumbe kwamba watumie fursa iliyopo kwa kuanzisha nishati mbadala.Tunafahamu Serikali imezuia mifuko ya plastiki ,hivyo vijana wanayo nafasi kutengeneza mfuko mbadala na hatimaye wakajiongezea kipato,"amesema.

Ameongeza kuwa kuna fursa ambazo zinakuja na mabadiliko ya tabia nchini huku akitoa mfano kuwa wananchi wanatakiwa kutumia mkaa mbadala ya kuendelea kukata miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

"Kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuna majukumu tunayoendelea nayo kupitia miradi mbalimbali.Hivyo mbali ya kujikita kwa vijana tumeanzisha vikundi vya wanawake na wanaume kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira nchini.

"Tunavyo vikundi 20 na kila kikundi kina watu kati ya watu 30 mpaka watu 50, na hao wanajihusisha na usafi wa mazingira kwa kukusanya taka na kisha taka hizo kutumika kuzalisha nishati mbadala na bidhaa nyingine zitokanazo na taka," amesema Muna.

Amefafanua katika kuhakikisha vikundi hivyo vinawajibika ipasavyo ,FORUMCC imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanavikundi hao, kuwapatia vifaa na soko la kuuzia bidhaa ambazo zinatokana na taka wanazokusanya na hiyo ni kwa Ilala.

"Licha ya kuwa  Ilala kwa hapa Dar es Salaam,pia tupo mkoani Singida ambako kule tupo kwenye kata tatu za Kijota,Mrama na Mtinko ambako wananchi wa maeneo hayo tunawasaidia katika kulima kilimo ambacho kinahimili athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mbali na kufanya kazi na vikundi,FORUMCC imekuwa ikihakikisha suala la uwajibikaji kuanzia kwa wananchi, serikali,sekta za umma na binafsi ambapo kila mmoja anatakiwa kuwajibika kukabiliana na mabadiliko yabtabianchi kwa kuwa na teknolojia rafiki katika kutunza mazingira.

"  Tumekuwa tukikuza uwajibikaji kwa watoa maamuzi na wapanga mipango na watunga sera.Tunatamani kuona kwenye mipango yao kunakuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na mazingira kwa ujumla.

"Na kwa ngazi ya Taifa FORUMCC tunahakikisha tunafuatilia kwa karibu  bajeti zote zinazohusu mazingira kama zinakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.Hata hivyo uwepo wa sera na sheria tunaamini utasaidia kuongeza uwajibikaji," amesema Muna na kuongeza "Kwa ujumla tunayo miradi mingi ambayo tunaifanya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
 Washindi wa pili wa michuano ya Kombe la mazingira kutoka timu ya Kajenjere wakiwa na kombe lao wakionesha furaha yao mbele ya viongozi wa Manispaa ya Ilala na FORUMCC
Msemaji wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu ( kulia)akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna wakifurahia jambo baada ya timu ya Abby FC kutangazwa kuwa mabalozi wa mazingira baada ya mashinda Kombe la mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...