NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

UGONJWA wa homa ya dengue ,umeingia mkoani Pwani ambapo hadi sasa wagonjwa 42 wameripotiwa kuugua hivyo kusababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa iliyokumbwa na ugonjwa huo.

Wilaya zilizokumbwa na ugonjwa huo ni pamoja na Mkuranga wagonjwa 35,Rufiji wanne na Kibaha Mji watatu.

Akizungumza,wakati wa  kikao maalum cha kamati ya ulinzi na usalama,kilichoshirikisha kamati ya amani na wadau mbalimbali kujadili juu ya hali hiyo mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,alieleza mgonjwa wa kwanza aligundulika mei 8 mwaka huu.

"Hakuna kifo kilichoripotiwa ,wagonjwa waliougua ni 42,tukizungumzia dengue tusisahau na kuweka mikakati kudhibiti na kipindupindu "

Ndikilo alizitaka kamati za afya wilaya kuupa kipaombele ugonjwa huu na kufanya vikao kujadili suala hili ilihali wananchi wapate taarifa sahihi ya ugonjwa huo ,dalili zake na namna ya kutibiwa.

Aliwaelekeza viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuwapa elimu waumini wao kuhusu ugonjwa wa homa ya dengue.

Nae Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Gunini Kamba alifafanua ugonjwa huu uliingia mwaka 2014 na kuugua wagonjwa 400 ila kipindi hiki kimezidi kufikia wagonjwa 3,609.

Aliwaasa wananchi ,wakiwa na dalili za homa wakimbilie vituo vya afya kujua hali zao na waachane na imani potofu kukimbilia kwa waganga.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama,aliwataka wananchi washirikiane na serikali kudhibiti gonjwa hilo ikiwemo kutunza mazingira na kupulizia dawa maeneo ya kutuama maji.

Ugonjwa wa dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virusi vya ugonjwa huo na dalili zake kuu ni homa kali ya ghafla,kuumwa kichwa sehemu za machoni na maumivu makali ya misuli na viungo vya mwili ,kutapika na uchovu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...