KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imekamilisha usajili wa winga Idd Seleman 'Nado', kutoka Mbeya City.

Nado ambaye ataanza kuitumikia timu hiyo msimu ujao, amesaini mkataba wa miaka miwili leo jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' na Mratibu wa timu, Phillip Alando.

Usajili wa winga huyo aliyeifungia Mbeya City mabao 10 msimu uliopita, ni sehemu ya mapendekezo ya Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Etienne Ndayiragije.

Huo ni usajili wa kwanza mpya kwa Azam FC, ambayo kwa mujibu wa ripoti ya kocha mpya, anahitaji nyota wapya wanne tu, wawili wakiwa wazawa na wawili kutoka nje.

Nado anatarajia kuungana na wachezaji wengine wa Azam FC waliopo kwenye kikosi hicho, katika maandalizi ya msimu mpya yatakayoanza Alhamisi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...