Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Chama cha Internet Society  Tanzania (ISOC) kimesema kuwa kutokana na mabadiliko ya Teknolojia katika Mitandao ya Jamii kunahitaji kuangalia namna ya kutumia mitandao hiyo katika manufaa ya kiuchumi pamoja kupata elimu katika Jamii tunayoishi.

 Chama hicho kimenzishwa katika kutoa elimu ya Mawasiliano ya Mitandao ya Jamii ikiwa ni pamoja na kuangalia maeneo ambayo hayapati huduma hizo kuweza kusaidia kupata utumiaji wa simu zao mitandao ya Jamii.

Akizungumza katika  warsha ya kuwajengea uwezo  waandishi habari katika matumizi ya Mitandao ya Jamii Mwenyikiti wa Chama hicho Mhandisi Abibu Ntahigiye amesema waandishi ni daraja katika jamii kwa kuweza kupata taarifa mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya nchi kwa kutumia vyombo vya habari.

Amesema kuwa matumizi ya Mitandao ya jamii baadhi wanaitumia vibaya kwa kutuma vitu visivyo na manufaa kwa jamii na wakati mwingine inaharibu vijana ambao wadogo kuiga vitu visivyo manufaa kwa taifa hadi Jamii.

Ntahigiye amesema kuwa matumizi ya Mitandao ya jamii imefundishwe kuanzia shule za msingi ili kuelewa maana ya matumizi hayo katika kuangalia manufaa wanayopata katika maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa serikali inakwenda kasi katika kutumia mitandao hali ambayo itafika wakati kila mtu anapata huduma katika Mitandao ambayo itasaidia kuondoa vitendo vya rushwa vinavyosababishwa watoa huduma kukutana na mwananchi.

Amesema baadhi ya nchi zimeanza kufundisha wanafunzi namna ya kutumia mitandao kwa kusisitiza kuwa pitia mara mbili kabla ya kutuma taarifa.

Amesema kutokana na matumizi mabaya ya Mitandao ya Jamii inafanya baadhi ya vijana kukosa sifa za kuajirika kutokana katika matumizi mabaya ya Mitandao kwa kutuma picha ambazo hazina maadili pamoja na kuandika vitu visivyofaa katika jamii inayowazunguka.

Nae Katibu Mkuu wa Chama hicho Nazarius Kirama amesema kuwa kutumia ISOC wameweza kujenga mnara kwa kutumia kikundi wilayani Kondoa ili kuwezesha kutumia mitandao ya jamii.
Amesema kuwa malengo ya ISOC ni kutaka kuhakikisha jamii yote inafikiwa na mitandao ya jamii katika kupata habari za manufaa ya elimu.

"Hatuwezi kuacha jamii inayotumia mitandao bila manufaa kwa kutuma au kusambaza taarifa za uongo ambazo haziwezi kusaidia maendeleo ya nchi"amesema Kirama.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Taasisi inayojishughulisha katika Uhamasishaji  Makundi yaliyopenzoni (TIBA) Marcela Lungu amesema kuwa baadhi ya picha chafu za wanawake zilizo katika Mitandao ya Jamii hazitumwi na wanawake wenyewe bali zinatumwa na wanaume.
Amesema kuwa matumizi ya Mitandao ya jamii kunahitajika elimu kwani baadhi ya wanawake hawazi kutangaza biashara zao katika mitandao ya jamii na kufanya biashara hizo kushindwa kueleka ndani jamii wanayoizunguka.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Internet Sociaty (Tanzania ISOC) Nazarius Kirama akitoa maelezo kuhusiana na utumiaji wa mitandao ya jamii kwa nia ya kujenga maadili ya nchi katika warsha uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha katika Uhamasishaji Makundi yaliyopenzoni (TIBA) Marcela Lungu akitoa namna ya wanawake kuwa nyuma katika mitandao ya jamii na kukosa baadhi ya fursa wakati warsha ya waandishi habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkufuzi kutoa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)  Damas Makweba akitoa namna ya matumizi ya Mitandao ya Jamii
 Mwenyikiti wa Chama Internet Sociaty Tanzania (ISOC) Mhandisi Abibu Ntahigiye akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya kuwajengea uwezo nna ya kutumia mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wakiwa katika warsha ya kujengewa uwezo.
Picha ya pamoja watendaji wa ISOC pamoja na waandishi habari walioshiriki warsha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...